Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi amewasihi watumishi wa ofisi yake kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha binafsi kwa kuwa huonesha tabia ya mtu haraka katika jamii.
Bw. Mkomi alisema hayo Novemba 24, 2025 wakati alipokuwa akiongea na
watumishi wa ofisi yake mara baada ya kupata mafunzo ya usimamizi wa fedha
binafsi yaliyotolewa na Mtoa Elimu wa Masuala ya Fedha (CFE) Bw. Edmund Munyagi
katika Ofisi za Utumishi zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
“Natoa rai kwa kila mtumishi wa ofisi hii kuhakikisha anajitahidi
kudhibiti matumizi ya fedha binafsi ili yasizidi kipato na kutumia akiba inayobaki
katika matumizi muhimu kuwekeza katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja kwa
manufaa baadae” alisema Bw. Mkomi.
Aliongeza kuwa wataalamu wa fedha wanasisitiza kuwekeza
katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja ili kukuza vipato na ni njia bora ya
kukuza mtaji wa mtu binafsi kwa kutumia njia za kitaalamu.
Naye, Mtoa Elimu ya Masuala ya Fedha (CFE) Bw. Edmund Munyagi
alibainisha kuwa tabia ya binadamu imejificha sana ingawa, fedha inaweza
kuonesha tabia ya mtu kwa haraka.
“Ukitaka kujua tabia ya mtu haraka apate fedha ili
aonekane namna anavyoitumia na jamii nzima itatambua kuwa mtu fulani amepata
fedha” alisema Bw. Munyangi.
Pia, alisema kuwa Mifuko ya uwekezaji wa pamoja hukusanya
fedha kutoka kwa wawekezaji wengi na kuziwekeza kwenye hisa, dhamana, au mali
nyingine ili kupunguza hatari ya kupotea na kuongeza faida kwa wawekezaji.
Ofisi ya Rais UTUMISHI imeweka utaratibu wa kutoa mafunzo mbalimbali kila
siku ya Jumatatu kwa watumishi wake ili
kuboresha utendaji kazi.
Watumishi wa Ofisi ya Rais UTUMISHI wakifuatilia kwa makini mada ya Usimamizi wa Fedha Binafsi na Uwekezaji kutoka kwa Mtoa Elimu wa Masuala ya Fedha (CFE) Bw. Edmund Munyagi katika eneo la mafunzo la Ofisi za Utumishi zilizopo Mtumba jijini Dodoma tarehe 24 NNovemba, 2025.
Baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Ofisi ya Rais UTUMISHI wakifuatilia kwa makini mada ya Usimamizi wa Fedha Binafsi na Uwekezaji kutoka kwa Mtoa Elimu wa Masuala ya Fedha (CFE) Bw. Edmund Munyagi (Hayupo pichani) katika eneo la mafunzo la Ofisi za Utumishi zilizopo Mtumba jijini Dodoma tarehe 24 NNovemba, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (wa Kwanza kushoto) akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu Bw. Xavier Daudi, viongozi na watumishi wengine wakifuatilia mada ya Usimamizi wa Fedha Binafsi yaliyotolewa na Mtoa Elimu wa Masuala ya Fedha (CFE) Bw. Edmund Munyagi (hayupo pichani) katika Ofisi za Utumishi zilizopo Mtumba jijini Dodoma tarehe 24 Novemba, 2025
Viongozi na Watumishi wa Ofisi ya Rais UTUMISHI wakifuatilia kwa makini mada ya Usimamizi wa Fedha Binafsi na Uwekezaji kutoka kwa Mtoa Elimu wa Masuala ya Fedha (CFE) Bw. Edmund Munyagi (Hayupo pichani) katika eneo la mafunzo la Ofisi za Utumishi zilizopo Mtumba jijini Dodoma tarehe 24 NNovemba, 2025.
No comments:
Post a Comment