Wednesday, November 26, 2025

WATUMISHI WA UMMA WAKUMBUSHWA KUZINGATIA MAADILI KATIKA UTENDAJI KAZI ILI KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

 

Na Antonia mbwambo-Iringa

Tarehe 27 Novemba,2025


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray ametoa wito kwa Watumishi wa Umma nchini kuzingatia maadili ya utendaji katika utekelezaji wa majukumu yao ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Mhe. Qwaray ameyasema hayo leo tarehe 27 Novemba, 2025 wakati akifungua kikao kazi kilichoshirikisha Maafisa Rasilimaliwatu na Maafisa Sheria kutoka taasisi za Serikali kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa Sheria namba 298 ya Utumishi wa Umma na kanuni zake.

“Watumishi wa Umma mzingatie maadili na kufuata Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyowekwa kwa mujibu wa Sheria ili kuondokana na changamoto katika utoaji wa huduma bila kujali unayemhudumia unamfahamu au haumfahamu kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi kwa manufaa ya Umma.

Aidha Mhe, Qwaray amesisitiza kwamba, kila Mtumishi wa Umma ana wajibu wa kuepusha migogoro na malalamiko mahali pa kazi lakini pia kuutendea haki muda waliopewa na serikali katika kuhudumia wananchi.

Vilevile, Naibu Waziri Qwaray ametoa wito kwa watumishi wa Umma kutumia rasilimali zilizopo ipasavyo kwa kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu na kwa wakati na kushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Awali, akitoa neno la utangulizi, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bi. Hilda Kabissa amesema kikao kazi hicho kimelenga kuchambua utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma ili kuimarisha utendaji kazi na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kwa Upande wake, Mwakilishi wa Katibu Mkuu ambaye ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi Felista Shuli wakati akimkaribisha Naibu Waziri kufungua kikao kazi hicho amesema kumekuwa na ukiukwaji wa Kanuni, Miongozo, Taratibu na Nyaraka mbalimbali zinazoandaliwa kwa ajili ya kuwapa mwongozo  Watumishi wa Umma hivyo, kupitia kikao kazi hicho kitawezesha Watumishi kuwa na uelewa juu ya Sheria na Kanuni hizo kwa lengo la kuongeza uwajibikaji wenye tija.

 

 




Naibu waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray (aliyeshikanisha mikono) akiwasili kwa ajili ya ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa Sheria na Maafisa Utumishi kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa jijini Dodoma.


Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray (wa tatu kulia)akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine aliokuwa nao meza kuu kabla wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Maafisa Utumishi na Maafisa Sheria Leo tarehe 27 N0vemba , 2025 mjini Iringa.

Maafisa Sheria na Maafisa Utumishi wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wawezeshaji (hawapo pichani)wakati wa kikao kazi kilicholenga kubadilishana uzoefu juu ya changamoto za utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na kanuni zake leo tarehe 27 Novemba,2027 mkoani Iringa

Naibu waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray akifuatilia uwasilishwaji wa mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa na Maafisa Utumishi na Maafisa Sheria wakati wa kikao kazi cha kilicholenga kubadilishana uzoefu juu ya changamoto za utekelezaji wa Sheria ya Utunishi wa Umma na kanuni zake leo tarehe 27 Novemba, 2025



Maafisa Sheria na Maafisa Utumishi wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wawezeshaji (hawapo pichani)wakati wa kikao kazi kilicholenga kubadilishana uzoefu juu ya changamoto za utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na kanuni zake leo tarehe 27 Novemba,2027 mkoani Iringa

Naibu waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray akizungumza na Maafisa Sheria na Maafisa Utumishi wakati akifungua kikao kazi kilicholenga kuchambua utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na kanuni zake ili kuimarisha utendaji kazi na kutoa huduma bora kwa wananchi leo tarehe 27 Novemba, 2025

Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bi. Hilda Kabissa (aliyekaa katikati)  akifuatilia
hotuba ya mgeni Rasmi ambaye ni Naibu waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Maafisa utumishi na Maafisa Sheria kilichofanyika mkoani Iringa tarehe 27 Novemba, 2025. Kulia kwake ni  Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Bi Felista Shuli na kushoto kwake ni Mkurugenzi
wa Huduma za Sheria  kutoka Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Charles R. Mulamula

Mbunge wa Iringa Mjini Mhe. Fadhili Ngajilo (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na katibu Tawala mkoa wa Iringa Bi Doris Kalasa (wa kwanza kushoto) na pamoja na mshiriki kutoka kutoka Ofisi ya Rais Ikulu Bi. Hilda Lugembe wakati wa kikao kazi cha maafisa Utumishi na Maafisa Rasilimali watu kilichofanyika tarehe 27 Novemba, 2025 Iringa mjini.



No comments:

Post a Comment