Sunday, November 16, 2025

WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUWA WAZALENDO ILI KUDUMISHA AMANI YA NCHI

 

Na Antonia Mbwambo-Dodoma

Tarehe 17.11.2025

 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi, ametoa wito kwa watumishi wa Ofisi hiyo, kuwa wazalendo wenye kuipenda nchi yao na rasilimali zilizopo ndani yake, ikiwa ni pamoja na kuepuka vitendo vya ugaidi na misimamo mikali inayotokana na ushawishi kutoka makundi yasiyofaa ambayo hupotosha umma na kuliingiza taifa katika vurugu na ukosefu wa amani.

Katibu Mkuu Mkomi ameyasema hayo leo tarehe 17/11/2025 alipokuwa akizungumza na watumishi wa Ofisi anayoingoza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji watumishi hao yanayofanyika katika eneo maalum la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma.

Aidha, Bw. Mkomi amewaasa Watumishi wa Umma kuendelea na uwajibikaji wenye kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia misingi ya maadili inayowaongoza kama Uzalendo, Uaminifu na Mteja kwanza ili kukidhi mahitaji ya wananchi na kuondoa tofauti zilizopo kati ya serikali na wananchi kwa ustawi wa Taifa.

“Uwajibikaji na Amani ni vitu vinavyoenda sambamba katika kujenga jamii bora na imara, kila mtumishi anapotekeleza wajibu wake kwa dhati, hujenga  msingi mzuri wa amani kwa kuwa amani inahitaji ushirikiano wa pamoja katika kutatua changamoto za wananchi na hivyo jamii kuwa na uwezo wa kukua na kuwa na maendeleo endelevu” alisema Bw. Mkomi.

Awali akiwasilisha mafunzo hayo, Mwezeshaji ambaye ni Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Polisi Mkoa wa Dodoma ASP Christer Kayombo ameeleza sababu mbalimbali zinazopelekea kuwepo kwa vitendo vinavyosababisha ukosefu wa amani, ikiwa ni pamoja na upotoshaji kupitia mitandao ya kijamii, uvivu pamoja na watoto kukosa misingi bora ya malezi wakiwa wadogo na hivyo kukua na hali ya ujasiri wa kufanya maovu hayo bila hofu.

ASP Kayombo alihitimisha mafunzo hayo kwa kutoa wito kwa Watumishi wa Umma na wananchi wote kwa ujumla kuungana kwa sauti moja katika kuhamasisha amani ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya namna ya kuepuka vitendo viovu vitakavyosababisha uvunjifu wa amani na kukemea vitendo hivyo kwa maslahi ya Taifa.


Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa UmmaSACP. Ibrahim Mahumi, akimshukuru Katibu Mkuu (kwa niaba ya mapolisi wote waliopo Ofisi hiyo na watumishi wote) kwa kutoa fursa ya kupata mafunzo hayo ya kila jumatatu kwa lengo la kuwajengea watumishi uwezo wa kiutendaji katika majukumu yao ya kila siku baada ya mwezeshaji kuhitimisha mafunzo hayo yalifanyika katika eneo la Ofisi hiyo lililopo Mtumba Jijini Dodoma leo tarehe 17/11/2025.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (wa kwanza kushoto) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Xavery Daudi (wa tatu kulia) wakati wakiendelea na mafunzo ya kuwajengea watumishi uwezo ambayo hufanyika kila jumatatu, yaliyotolewa na Mwezeshaji ambaye ni Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Polisi Mkoa wa Dodoma ASP Christer Kayombo katika eneo la Ofisi hiyo lililopo Mtumba Jijini Dodoma leo tarehe 17/11/2025.

Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo katika utendaji wao ambayo hufanyika kila jumatatu katika eneo maalum lililopo kwenye Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma leo tarehe 17/11/2025.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (aliyesimama mbele) akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo katika eneo maalumu la kutolea mafunzo ya kuwajengea uwezo baada ya mwezeshaji  kuhitimisha mafunzo hayo leo tarehe 17/11/2025 Mtumba jijini Dodoma

Mwezeshaji ambaye ni Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Polisi Mkoa wa Dodoma ASP Christer Kayombo (aliyesimama mbele) akitoa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora yaliyolenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji ambayo yalifanyika katika eneo la Ofisi hiyo lililopo Mtumba Jijini Dodoma leo tarehe 17/11/2025.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa UmmaSACP. Ibrahim Mahumi, akimshukuru Katibu Mkuu (kwa niaba ya mapolisi wote waliopo Ofisi hiyo na watumishi wote) kwa kutoa fursa ya kupata mafunzo hayo ya kila jumatatu kwa lengo la kuwajengea watumishi uwezo wa kiutendaji katika majukumu yao ya kila siku baada ya mwezeshaji kuhitimisha mafunzo hayo yalifanyika katika eneo la Ofisi hiyo lililopo Mtumba Jijini Dodoma leo tarehe 17/11/2025.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw.Musa Magufuli akimshukuru mwezeshaji kwa mafunzo aliyoyatoa na kumkaribisha Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa UmmaSACP. Ibrahim Mahumi, ili aseme neno kwa niaba ya mapolisi wote waliopo Ofisi hiyo na watumishi wote kutokana na mafunzo hayo yaliyofanyika katika eneo la Ofisi hiyo lililopo Mtumba Jijini Dodoma leo tarehe 17/11/2025

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Polisi Mkoa wa Dodoma ASP Christer Kayombo akiwaelezea kwa vitendo watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI namna ya kujitetea ili kujinasua wanapokutana na vitendo uonevu au vitakavyosababisha uvunjifu wa amani leo tarehe 17/11/2025 katika eneo la Ofisi hiyo lililopo Mtumba Jijini Dodoma.

Baadhi ya wakurugenzi na wakurugenzi wasaidizi kutoka Idara na vitengo mbalimbali vya Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia mada iliyokuwa ikiendelea katika mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo katika utendaji wao ambayo hufanyika kila jumatatu katika eneo maalum lililopo kwenye Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma leo tarehe 17/11/2025.

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Polisi Mkoa wa Dodoma ASP Christer Kayombo (aliyesimama mbele) akitoa ufafanuzi wa namna ya kuepuka vishawishi vitakavyosababisha kuwepo kwa vitendo vya uvunjifu wa amani,wakati akitoa mafunzo hayo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma leo tarehe 17/11/2025.

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Polisi Mkoa wa Dodoma ASP Christer Kayombo (aliyesimama mbele) akiwaongoza watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI kuimba wimbo wa kukiri na kuahidi uaminifu katika kuilinda na kutetea nchi ya Tanzania na maslahi yake leo tarehe 17/11/2025 katika Ofisi hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma.









No comments:

Post a Comment