Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Cosmas Ngangaji amemshukuru Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala Bw. Musa Magufuli kwa ubunifu wake na kuweka utaratibu wa kuwapongeza na kuwatakia kila la kheri watumishi wake kwa kuzingatia mwezi waliozaliwa.
“Kwa niaba ya watumishi wenzangu tuliozaliwa mwezi Novemba
ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu wetu Bw. Juma Mkomi, tunashukuru kwa motisha hii
ya kufanya tukio la kumbukizi ya kuzaliwa kwetu kwa pamoja na kufurahi na
watumishi wenzetu” alisema Bw. Ngangaji
Aliongeza kuwa tabia njema huonekana kama ni ya
kawaida, lakini kwa tukio hili haina budi kupongeza wote waliofanikisha jitihada
hizi zenye kufurahisha jamii.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Anuai za Jamii kutoka Ofisi ya Rais-
UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo amewasisitiza wazaliwa wote wa mwezi Novemba kuzingatia
mafunzo waliyopata leo kuhusu usimamizi wa fedha binafsi na uwekezaji kwa kuwa
ni kipimo cha utu ambacho kinatakiwa kufikiwa na kila mmoja.
Aidha, amewapongeza wote waliozaliwa mwezi Novemba na
kuwatakia kila la kheri katika kumbukizi ya kuzaliwa kwao na kuwaomba waendelee
kutumikia familia zao na taifa kwa ufanisi.
Picha za Viongozi na watumishi mbalimbali wa Ofisi ya Rais UTUMISHI waliozaliwa Mwezi Novemba, wakilishwa Keki kama ishara ya upendo kwao.
No comments:
Post a Comment