Na. Veronica Mwafisi-Ruvuma
Tarehe 25 Novemba, 2025
Watumishi wa Umma wa Kituo cha Afya Kilagano
na Shule ya Sekondari Jenista Mhagama waliopo katika
Halmashauri ya Wilaya ya Songea wameishukuru Serikali kupitia Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing
Investments kwa kuanzisha Mradi wa Ujenzi wa Makazi kwa Watumishi wa Umma nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Watumishi hao, Mkuu wa Shule ya Sekondari
Jenista Mhagama, Bi. Felister Kulwambalo amesema, Watumishi wa Shule ya
Sekondari Jenista Mhagama wanaishukuru Serikali kupitia timu hiyo kwa
kusimamia, kukagua na kufanya tathmini ya mwisho ya
kukamilika kwa mradi huo na kuahidi watakapokabidhiwa
tija ya utendaji kazi itaongezeka.
“Tunaishukuru sana Serikali
kwa kuona umuhimu wa kutujengea makazi bora, tunaahidi tutakapokabidhiwa rasmi nyumba
hizi tija ya utendaji kazi itaongezeka sana, lakini pia adha ya watumishi
kutoka umbali mrefu kuja katika eneo la kazi itapungua,” amesema Bi. Kulwambalo
Timu hiyo ya Wataalam imeongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo
cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw.
Patrick Allute wakati wa ziara ya kikazi waliyoifanya
kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma kwa lengo la kukagua na kufanya tathmini ya mwisho ya kukamilika kwa
mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma utakaosaidia kuondokana na changamoto ya
makazi kwa watumishi hao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Mradi
huo wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma kwa
awamu ya kwanza umetekelezwa katika mikoa ya Dodoma,
Singida, Lindi, Pwani na Ruvuma.
Mwonekano
wa jengo la mradi wa makazi ya watumishi wa umma lililopo katika Kituo cha Afya
Kilagano, Halmashauri ya Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma.
Kaimu
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na
Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (aliyenyoosha mkono) akisisitiza jambo mara
baada ya Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Wizara
ya Fedha na Watumishi Housing Investments kukagua na kufanya tathmini ya mwisho
ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa makazi ya
Watumishi wa Umma katika Kituo cha Afya Kilagano, Halmashauri ya Wilaya
ya Songea, mkoani Ruvuma.
Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji kutoka Watumishi Housing Investments, Bw. Paskali Massawe (aliyenyoosha mkono) akizungumza
jambo wakati Timu ya wataalam kutoka Ofisi
ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing
Investments ilipofika
kukagua na kufanya tathmini ya mwisho ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma katika
Kituo cha Afya Kilagano, Halmashauri ya Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma. Wa
kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mipango na Bajeti, Bi. Julieth
Magambo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na
Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (kulia) na Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji kutoka Watumishi Housing Investments, Bw. Paskali Massawe (kushoto) wakimsikiliza Mganga
Mkuu wa Kituo cha Afya Kilagano (katikati) mara
baada ya timu hiyo kukagua na kufanya tathmini ya mwisho
ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa makazi ya
Watumishi wa Umma katika Kituo hicho kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya
Songea, mkoani Ruvuma.
Kaimu
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na
Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (aliyenyoosha kidole) akisisitiza jambo kwa Mkuu
wa Shule ya Sekondari Jenista Mhagama, Bi. Felister Kulwambalo (wakwanza
kushoto) wakati Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora,
Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments ilipokuwa ikikagua na kufanya
tathmini ya mwisho ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi
wa makazi ya Watumishi wa Umma katika Shule hiyo katika Halmashauri ya
Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma.
Mkurugenzi
Msaidizi Sehemu ya Mipango na Bajeti, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora,
Bi. Julieth Magambo (aliyevaa miwani) akizungumza jambo wakati wa ziara ya Timu
ya wataalam kutoka Ofisi hiyo, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments
kukagua na kufanya tathmini ya mwisho ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma katika Kituo cha
Afya Kilagano, Halmashauri ya Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma.
Kaimu
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na
Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (wakwanza kushoto), Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji kutoka Watumishi Housing Investments, Bw. Paskali Massawe (katikati) na Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya fedha, Bw. Ezekiel Odipo
(wakwanza kulia) wakizungumza jambo mara baada ya kukagua
na kufanya tathmini ya mwisho ya kukamilika kwa mradi wa
ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma katika Kituo cha Afya Kilagano,
Halmashauri ya Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma.
Timu
ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na
Watumishi Housing Investments ikiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa
Shule ya Sekondari Jenista Mhagama mara baada ya timu hiyo kukagua na kufanya
tathmini ya mwisho ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi
wa makazi ya Watumishi wa Umma katika shule hiyo iliyopo Halmashauri ya
Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma.
Timu
ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na
Watumishi Housing Investments ikijadili jambo mara baada ya kukagua na kufanya
tathmini ya mwisho ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi
wa makazi ya Watumishi wa Umma katika Shule ya Sekondari Jenista Mhagama,
Halmashauri ya Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma. Wengine ni Walimu wa Shule
hiyo.






No comments:
Post a Comment