Na. Veronica Mwafisi-Singida
Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments
ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute imefanya
ziara ya kikazi iliyolenga kukagua na kufanya tathmini ya mwisho ya kukamilika kwa
mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma wa
Shule ya Sekondari Maluga yanayojengwa katika Kijiji cha Maluga, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba na Zahanati ya Makunda, Kijiji
cha Makunda Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, mkoani Singida ambapo kukamilika
kwa mradi huo kutasaidia kuongeza tija Serikalini.
Akizungumza
kwa niaba ya timu hiyo mara baada ya kukagua mradi huo, Kaimu Mkurugenzi Allute amesema, makazi ya watumishi wa umma yanapokuwa
karibu na maeneo ya kazi huongeza ufanisi na uwajibikaji hivyo, utekelezaji wa mradi
huo kwa awamu ya kwanza katika mikoa ya Dodoma,
Singida, Lindi, Pwani na Ruvuma utamkomboa
mtumishi wa umma katika utendaji kazi.
“Maeneo ya pembezoni yamekuwa na changamoto ya makazi na
kusababisha baadhi ya watumishi wa umma kutokutekeleza majukumu yao kwa
ufanisi, kupitia mradi huu unaotekelezwa kwa awamu ya kwanza katika mikoa ya Dodoma,
Singida, Lindi, Pwani na Ruvuma unatarajiwa kuongeza
ufanisi na uwajibikaji kwa watumishi wa umma kwenye maeneo hayo,” amesema
Mkurugenzi Allute
Naye, Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mipango na Bajeti, Bi. Julieth
Magambo amesema ili makazi hayo yawe na ubora wa kudumu ni vema Watumishi
watakaoishi katika makazi hayo wakazingatia utunzaji wa miundombinu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
wa Fedha na Uwekezaji kutoka Watumishi Housing
Investments, Bw. Paskali Massawe,
amesema makazi hayo yamejengwa kwa kuzingatia ubora ili kuendana na malengo ya
Serikali katika kuwatengenezea mazingira bora watumishi wa umma.
Kadhalika,
Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya fedha, Bw. Ezekiel Odipo ameeleza
kuwa, ili kutimiza malengo ya Serikali ya kuongeza tija kwa watumishi wa umma fedha
nyingi imetolewa kwa lengo la kuboresha makazi ya watumishi hao ili waweze
kutoa huduma bora kwa ustawi wa taifa.
Mwonekano wa jengo la mradi wa makazi ya Watumishi wa
Umma lililopo katika Kijiji cha Makunda,
Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (aliyenyanyua mkono) akizungumza
jambo wakati Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments ikikagua
na kufanya tathmini ya mwisho
ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma katika Kijiji cha
Makunda, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, mkoani Singida. Wengine ni Watumishi
wa Zahanati ya Makunda.
Katibu wa Afya, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Bw. Sunday Mbonigaba (wakwanza
kushoto) akifafanua jambo kwa Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi
Housing Investments mara baada ya timu hiyo kukagua
na kufanya tathmini ya mwisho ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma katika Halmashauri hiyo
Kijiji cha Makunda mkoani Singida.
Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments ikiwa
katika picha ya pamoja na Watumishi wa Zahanati ya Makunda mara baada ya timu
hiyo kukagua na kufanya tathmini ya mwisho ya kukamilika kwa
mradi wa ujenzi wa
makazi ya Watumishi wa Umma katika Kijiji cha Makunda, Halmashauri ya Wilaya ya
Iramba, mkoani Singida.
Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments ikielekea
kukagua na kufanya tathmini ya mwisho ya kukamilika kwa
mradi wa ujenzi wa
makazi ya Watumishi wa Umma katika Kijiji cha Makunda, Halmashauri ya Wilaya ya
Iramba, mkoani Singida. Wengine ni Watumishi wa Zahanati ya Makunda.
Mwonekano wa jengo la mradi wa makazi ya Watumishi wa Umma
lililopo katika Kijiji cha Maluga, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute
(aliyenyoosha mkono) akisisitiza jambo mara baada ya kukagua na kufanya tathmini ya mwisho
ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma katika Kijiji cha
Maluga, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, mkoani Singida. Wengine ni Wakurugenzi
na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing
Investments.
Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Wizara ya Fedha na Watumishi Housing Investments
ikitazama makazi ya Watumishi wa Umma (hayapo pichani) katika Kijiji cha
Maluga, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, wakati ikikagua na
kufanya tathmini ya mwisho ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma mkoani Singida.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute
(wakwanza kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi
wa Fedha na Uwekezaji, Watumishi Housing
Investments, Bw. Paskali Massawe (kulia kwake) mara baada ya kukagua na
kufanya tathmini ya mwisho ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma katika Kijiji cha
Maluga, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.


No comments:
Post a Comment