Wednesday, November 29, 2017

IDARA YA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA YASHIRIKI KAMPENI KUELEKEA SIKU YA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU KITAIFA KWA KUPATIWA MAFUNZO YA MAADILI NA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Ukuzaji wa Maadili, Ofisi ya Rais - UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Leila Mavika (aliyesimama) akitoa mafunzo kuhusu maadili na mapambano dhidi ya rushwa kwa watumishi wa Ofisi ya Rais -Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Makao Makuu, ikiwa ni sehemu ya kampeni kuelekea Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa tarehe 10 Disemba, 2017.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais -Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Makao wakisikiliza kwa makini mafunzo kuhusu maadili na mapambano dhidi ya rushwa yaliyotolewa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Ukuzaji wa Maadili, Ofisi ya Rais - UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Leila Mavika (hayupo pichani), ikiwa ni sehemu ya kampeni kuelekea Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa tarehe 10 Disemba, 2017.

Mmoja wa watumishi wa Ofisi ya Rais -Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Makao akiuliza swali kuhusu maadili wakati wa kuhusu maadili na mapambano dhidi ya rushwa yaliyotolewa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Ukuzaji wa Maadili, Ofisi ya Rais - UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Leila Mavika (hayupo pichani), ikiwa ni sehemu ya kampeni kuelekea Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa tarehe 10 Disemba, 2017.

Monday, November 27, 2017

WAZIRI JAFO AKIZINDUA SIKU YA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU KITAIFA NCHINI

KUZINGATIA MAADILI NA KUPIGA VITA RUSHWA NDIO MSINGI MKUU WA MAENDELEO YA TAIFA LETU



Waziri wa Nchi - Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani S. Jafo (Mb) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Hazina Ndogo.

Waziri wa Nchi - Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani S. Jafo (Mb) akimkabidhi nyaraka kuhusu maadili mwakilishi wa Katibu Mkuu-UTUMISHI Bibi Janeth Mishinga wakati wa uzinduzi wa Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa nchini.

Sehemu ya washiriki waliohudhuria ufunguzi wa Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Hazina Ndogo wakimsikiliza mgeni rasmi, Waziri wa Nchi - Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani S. Jafo (Mb).

Baadhi ya wanafunzi waliowawakilisha wenzao wakati wa uzinduzi wa Klabu za Maadili Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Hazina Ndogo.