Tuesday, November 7, 2017

DKT. NDUMBARO AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUZINGATIA UADILIFU, KUJITUMA NA KUWAJIBIKA KWA WANANCHI

Add caption


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa maelekezo mbalimbali ya masuala ya kiutumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba  katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma.  Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hamashauri ya Wilaya ya Madaba Bw. Shafi Mpenda na kushoto kwakwe ni   Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Bw. Bwai Biseko.

Baadhi ya watumishi wa Hamashauri ya Wilaya ya Madaba wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) aliyoyatoa katika halmashauri hiyo, wakati ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma. 

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Bw.  Biseko  Bwai akitoa  taarifa ya utekelezaji wa  masuala ya kiutumishi kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo mkoani Ruvuma yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijiji Bw.   Simon Bulenganija akitoa taarifa ya utekelezaji wa masuala ya kiutumishi Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo mkoani Ruvuma,  yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini wa   Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Ibrahim Mahumi akitoa maelekezo kwa watumishi wa Halmashauri ya  Wilaya  ya Songea  Vijijini kuhusu taratibu zinazohusu  menejimenti ya  Rasilimaliwatu serikalini, wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro ya kuhimiza uwajibikaji.

Baadhi ya watumishi wa Hamashauri ya Wilay ya Songea Vijiji wakimsikiliza Katibu  Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya katibu mkuu huyo  ya kuhimiza uwajibikaji katika Hamashauri hiyo.


No comments:

Post a Comment