Friday, August 9, 2019

WANUFAIKA WA TASAF WILAYANI KARAGWE WAISHUKURU SERIKALI KWA KUWATHAMININaibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akilakiwa na wananchi wa kijiji cha Rulalo katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini  katika kijiji cha Rulalo  juu ya utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiangalia zizi la mbuzi la mmoja wa Walengwa wa TASAF, Bi. Beatha Katushabe wa kijiji cha Rulalo wilayani Karagwe mkoani Kagera ambaye anamiliki mbuzi 25 aliowapata kutokana na ruzuku ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati) akipokea zawadi ya mkungu wa ndizi kutoka kwa Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Rukole, Wilayani Karagwe mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Rukole, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, Bi. Rhoda Ernest (wa tatu kushoto kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akionyesha kisima cha kuvuna maji ya mvua alichokijenga kwa kutumia na ruzuku ya TASAF. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akipokea zawadi ya mkeka uliosukwa na mmoja wa wanufaika wa TASAF, Bi.Rhoda Ernest katika kijiji cha Rukole, wilayani Karagwe Mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Thursday, August 8, 2019

SERIKALI YAWATAKA MAAFISA UGANI NCHINI KUTOA HUDUMA YA KITAALAMU KWA WANANCHI ILI KULETA MATOKEO CHANYA KATIKA SEKTA YA KILIMO, UVUVI NA UFUGAJINaibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ambaye ni Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Kagera akielekea kukagua mabanda ya maonyesho katika Viwanja vya Kyakailabwa mkoani Kagera. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Brigedia Jenerali Marco Gaguti.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ambaye ni Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Kagera akiangalia mboga katika shamba darasa la Jeshi la Magereza lililopo Viwanja vya Kyakailabwa mkoani Kagera.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ambaye ni Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Kagera akiangalia chakula cha samaki katika bwawa la kufugia samaki la Jeshi la Magereza Kagera lililopo Viwanja vya Kyakailabwa mkoani Kagera.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ambaye ni Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Kagera akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kagera (hawapo pichani) katika Viwanja vya Kyakailabwa mkoani Kagera.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ambaye ni Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Kagera akitunuku cheti na zawadi kwa watumishi wa Kiwanda cha Sukari Kagera ambao ni washindi wa pili wa jumla wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima katika Viwanja vya Kyakailabwa mkoani Kagera.

Wednesday, August 7, 2019

WANUFAIKA WA TASAF WILAYANI NGARA WASHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA MIRADI YA KUTOA AJIRA YA MUDA
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wananchi na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kijiji cha Mayenzi wilayani Ngara wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Ngara (Kulia), Mhe. Alex Gashaza na Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mhe. Luteni Kanali Michael Mtenjele wakielekea kukagua shamba la miti lililopandwa na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia utaratibu wa Miradi ya Ajira ya Muda katika Kijiji cha Mayenzi wilayani Ngara mkoani Kagera.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa na Viongozi wa Wilaya ya Ngara wakikagua shamba la miti aina ya mikaratusi lililopandwa na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia utaratibu wa Miradi ya Ajira ya Muda katika Kijiji cha Mayenzi wilayani Ngara mkoani Kagera.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akipokelewa kwa burudani ya ngoma na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini alipowasili katika Kijiji cha Murugina wilayani Ngara kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. Alex Gashaza.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akicheza ngoma na wananchi na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini alipowasili katika Kijiji cha Murugina wilayani Ngara kukagua utekelezaji wa miradi ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.


Monday, August 5, 2019

SERIKALI YAWEKA MKAKATI KUHAKIKISHA WANUFAIKA WA TASAF WANAPATA RUZUKU STAHIKI NA KWA WAKATI


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kijiji cha Magata, wilayani Muleba mkoani Kagera wakati wa ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Magata baada ya kumaliza mkutano na wananchi na wanufaika wa TASAF katika Kijiji cha Magata, wilayani Muleba mkoani Kagera. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhe. Mhandisi Richard Ruyango na baadhi ya Watendaji wa TASAF wakielekea kwenye nyumba ya mnufaika wa TASAF kuona namna alivyotumia ruzuku inayotolewa na Serikali kupitia mfuko huo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa na moja ya familia ya mnufaika wa TASAF katika Kijiji cha Magata wilayani Muleba ambaye alipata ulemavu wa viungo kutokana na ajali.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiangalia banda la mifugo katika Kaya ya mmoja wa wanufaika wa TASAF, Bi. Nazifa Naziru katika Kijiji cha Magata wilayani Muleba.

Sunday, August 4, 2019

DKT. MWANJELWA AWATAKA WANUFAIKA WA TASAF WENYE NGUVU WAFANYE KAZI BADALA YA KUSUBIRI RUZUKUNaibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akilakiwa na wananchi wa kijiji cha Burugo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera ambako yuko kwenye ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kukutana na Watumishi wa Umma kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wananchi na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini  katika kijiji cha Burugo (hawapo pichani) juu ya utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Baadhi ya Wananchi na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika katika kijiji cha Lukindo kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani).

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati) akiwa nyumbani kwa mmoja wa walengwa wa TASAF katika kijiji cha Burugo Bi. Justa Migini (kulia kwa Naibu Waziri),wa kwanza kushoto ni Meneja wa Miradi ya Ajira za Muda TASAF Bw. Paul Kijazi  wakishuhudia nyumba iliyojengwa na mlengwa huyo kwa kutumia ruzuku ya TASAF.

Mmoja wa Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa  kijiji cha Burugo, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera Bi. Agnes Kemilembe akitoa ushuhuda wa namna alivyotumia ruzuku kuboresha makazi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb). 

Mmoja wa Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Burugo, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera Bi. Agnes Kemilembe akimuonyesha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) shamba lake analoliendeleza kwa kutumia ruzuku ya TASAF.

Friday, August 2, 2019

WAAJIRI NCHINI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU WANAPOWASILISHA TAARIFA ZA KIUTUMISHI OFISI YA RAIS UTUMISHI ILI KUEPUKA MALALAMIKO YA WATUMISHINaibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Kagera (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.


Baadhi ya Watumishi wa Umma mkoani Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof. Faustin Kamuzora akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na Watumishi wa Umma mkoani Kagera chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.