Sunday, August 4, 2019

DKT. MWANJELWA AWATAKA WANUFAIKA WA TASAF WENYE NGUVU WAFANYE KAZI BADALA YA KUSUBIRI RUZUKU



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akilakiwa na wananchi wa kijiji cha Burugo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera ambako yuko kwenye ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kukutana na Watumishi wa Umma kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wananchi na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini  katika kijiji cha Burugo (hawapo pichani) juu ya utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Baadhi ya Wananchi na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika katika kijiji cha Lukindo kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani).

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati) akiwa nyumbani kwa mmoja wa walengwa wa TASAF katika kijiji cha Burugo Bi. Justa Migini (kulia kwa Naibu Waziri),wa kwanza kushoto ni Meneja wa Miradi ya Ajira za Muda TASAF Bw. Paul Kijazi  wakishuhudia nyumba iliyojengwa na mlengwa huyo kwa kutumia ruzuku ya TASAF.

Mmoja wa Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa  kijiji cha Burugo, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera Bi. Agnes Kemilembe akitoa ushuhuda wa namna alivyotumia ruzuku kuboresha makazi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb). 

Mmoja wa Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Burugo, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera Bi. Agnes Kemilembe akimuonyesha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) shamba lake analoliendeleza kwa kutumia ruzuku ya TASAF.

No comments:

Post a Comment