Saturday, August 31, 2019

SERIKALI KUWASILISHA MUSWADA BUNGENI WA KUWA NA MAMLAKA YA SERIKALI MTANDAO



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst.) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na Wataalam wa ndani wa TEHAMA (hawapo pichani) waliotengeneza Mfumo mpya wa Taarifa Shirikishi za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) na Mfumo wa Wazi wa Tathmini ya Utendaji Kazi wa  Kieletroniki (eOPRAS) ambayo inatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst.) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiwahimiza Wataalam wa ndani wa TEHAMA (hawapo pichani) waliotengeneza Mfumo mpya wa Taarifa Shirikishi za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) na Mfumo wa Wazi wa Tathmini ya Utendaji Kazi wa  Kieletroniki (eOPRAS) kuhakikisha wanakamilisha utengenezaji wa mifumo hiyo kwa ufanisi ili iwe na manufaa ya kiutendaji Serikalini.

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA), Dkt. Jabir K. Bakari akimuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst.) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) namna Serikali Mtandao inavyofanya kazi, wakati waziri huyo alipoitembelea wakala hiyo kuhimiza uwajibikaji.

Sehemu ya muonekano wa Mfumo mpya wa Taarifa Shirikishi za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) uliotengenezwa na Wataalam wa ndani wa TEHAMA ambao unatarajiwa unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.


No comments:

Post a Comment