Friday, August 9, 2019

WANUFAIKA WA TASAF WILAYANI KARAGWE WAISHUKURU SERIKALI KWA KUWATHAMINI



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akilakiwa na wananchi wa kijiji cha Rulalo katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini  katika kijiji cha Rulalo  juu ya utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiangalia zizi la mbuzi la mmoja wa Walengwa wa TASAF, Bi. Beatha Katushabe wa kijiji cha Rulalo wilayani Karagwe mkoani Kagera ambaye anamiliki mbuzi 25 aliowapata kutokana na ruzuku ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati) akipokea zawadi ya mkungu wa ndizi kutoka kwa Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Rukole, Wilayani Karagwe mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Rukole, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, Bi. Rhoda Ernest (wa tatu kushoto kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akionyesha kisima cha kuvuna maji ya mvua alichokijenga kwa kutumia na ruzuku ya TASAF. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akipokea zawadi ya mkeka uliosukwa na mmoja wa wanufaika wa TASAF, Bi.Rhoda Ernest katika kijiji cha Rukole, wilayani Karagwe Mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

No comments:

Post a Comment