Wednesday, August 7, 2019

WANUFAIKA WA TASAF WILAYANI NGARA WASHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA MIRADI YA KUTOA AJIRA YA MUDA




Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wananchi na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kijiji cha Mayenzi wilayani Ngara wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Ngara (Kulia), Mhe. Alex Gashaza na Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mhe. Luteni Kanali Michael Mtenjele wakielekea kukagua shamba la miti lililopandwa na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia utaratibu wa Miradi ya Ajira ya Muda katika Kijiji cha Mayenzi wilayani Ngara mkoani Kagera.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa na Viongozi wa Wilaya ya Ngara wakikagua shamba la miti aina ya mikaratusi lililopandwa na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia utaratibu wa Miradi ya Ajira ya Muda katika Kijiji cha Mayenzi wilayani Ngara mkoani Kagera.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akipokelewa kwa burudani ya ngoma na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini alipowasili katika Kijiji cha Murugina wilayani Ngara kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. Alex Gashaza.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akicheza ngoma na wananchi na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini alipowasili katika Kijiji cha Murugina wilayani Ngara kukagua utekelezaji wa miradi ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.


No comments:

Post a Comment