Thursday, November 13, 2025

Monday, November 10, 2025

KATIBU MKUU OFISI YA RAIS AWASISITIZA WATUMISHI WA UMMA KUDUMISHA AMANI

Na Eric Amani, Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi, ametoa wito kwa Watumishi wa Umma nchini kuendelea kudumisha amani, mshikamano na uzalendo katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa manufaa ya Taifa.

Akizungumza jijini Dodoma leo tarehe 10 Novemba, 2025 wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo yanayofanyika kila siku ya Jumatatu, Katibu Mkuu Mkomi amesema, Utumishi wa Umma una nafasi kubwa katika kulinda na kuimarisha amani ya nchi kwa kutoa huduma bora, kuzingatia maadili ya kazi na kuepuka vitendo vinavyoweza kuleta mgawanyiko katika jamii.

“Watumishi wa Umma ni kioo cha Serikali, hivyo mnapaswa kuwa mfano katika uadilifu, uvumilivu na uzalendo,” alisema Katibu Mkuu Mkomi.

Bw. Mkomi pia aliwakumbusha watumishi kuzingatia misingi ya utawala bora, uwajibikaji, na matumizi sahihi ya rasilimali za umma, sambamba na kutumia lugha na mienendo inayojenga taswira chanya ya Serikali.

Kwa upande wake mwewezeshaji ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa TEHEMA, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mussa Chiwelenje amewasisitiza Watumishi kutunza taarifa zao binafsi, za Ofisi na kutochezea miundombinu ya TEHAMA kwa usalama wa Taifa.




Mkurugenzi Kitengo cha Usalama wa Mtandao na TEHAMA Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mussa Chiwelenje akiwasilisha Mada ya usalama wa Mtandao kwenye Mafunzo ya Kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi ya Rais - UTUMISHI Novemba 10, 2025.

  


Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais - UTUMISHI Bw. Mussa Magufuli Novemba 10, 2025 akichangia Mada kwenye mafunzo ya Kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini Ofisi ya Rais - UTUMISHI Bw. Priscus Kiwango Novemba 10, 2025 akichangia Mada ya usalama wa mtandao na hadaa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo Jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Mwezeshaji kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  alipofika kutoa mafunzo kuhusu usalama wa mtandao Novemba 10, 2025 Mtumba Jijini Dodoma.



Monday, November 3, 2025

Wednesday, October 29, 2025

WATENDAJI WAKUU OFISI YA RAIS-UTUMISHI WAPIGA KURA, KATIBU MKUU MKOMI ATOA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA NA WANANCHI KUJITOKEZA KUTIMIZA HAKI YAO YA KIKATIBA

 




WATENDAJI WAKUU OFISI YA RAIS-UTUMISHI WAPIGA KURA, KATIBU MKUU MKOMI ATOA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA NA WANANCHI KUJITOKEZA KUTIMIZA HAKI YAO YA KIKATIBA

Na. Antonia Mbwambo na Veronica Mwafisi -Dodoma

Tarehe 29 Oktoba, 2025

Watendaji Wakuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora leo tarehe 29.10.2025 wameshiriki zoezi la kupiga kura katika Vituo mbalimbali na kuchagua Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani.

Akishiriki zoezi hilo katika Kituo cha Kupiga Kura cha Msangalale Mashariki, Kata ya Dodoma Makulu, jijini Dodoma, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi ametoa wito kwa Watumishi wa Umma na Wananchi kujitokeza kuchagua viongozi wanaowahitaji kwa maendeleo ya Taifa.

“Namshukuru Mungu nimeshikiri salama zoezi hili muhimu la Kikatiba, nipende kutoa wito kwa Watumishi wa Umma na Wananchi kwa ujumla kushikiriki pia kwani ni haki yao ya msingi.” Bw. Mkomi amesisitiza.

Amesema hali katika Kituo hicho ni ya utulivu na wananchi wamekua wakimiminika kwenda kupiga kura hivyo amewasisitiza kila mwenye haki ya kushiriki zoezi hilo afanye hivyo.

Aidha, Bw. Mkomi amewapongeza Waratibu wa zoezi hilo katika Kituo hicho kwa kuonyesha ushirikiano kwa wananchi wanaoenda kushiriki katika zoezi hilo na kuhakikisha kila mwenye sifa anashiriki kikamilifu.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Xavier Daudi ameshiriki zoezi hili muhimu katika Kituo cha Mwatano, Kata ya Miyuji, Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akiweka fomu ya kupiga Kura katika sanduku la Kura mara baada ya kushiriki zoezi hilo la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Dodoma Makulu, Mtaa wa Msangalale jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akiweka fomu ya kupiga Kura katika sanduku la Kura mara baada ya kushiriki zoezi hilo la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa wa Mwatano jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (aliyesimama) akipokea fomu ya kushiriki kupiga Kura kutoka kwa Wasimamizi wa Uchaguzi katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Dodoma Makulu, Mtaa wa Msangalale jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (aliyesimama) akisubiri kupatiwa fomu ya kushiriki kupiga Kura kutoka kwa Wasimamizi wa Uchaguzi katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa wa Mwatano jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akionesha jina lake katika orodha ya wapiga Kura iliyobandikwa katika kituo hicho kabla ya kushiriki kupiga kura katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Dodoma Makulu, Mtaa wa Msangalale jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akishiriki kupiga Kura katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa wa Mwatano jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akionesha kadi yake ya kupiga Kura kabla ya kushiriki zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Dodoma Makulu, Mtaa wa Msangalale jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akihakiki jina na picha yake kwenye daftari la kudumu kabla ya kushiriki zoezi la kupiga Kura katika Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa wa Mwatano jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akipakwa wino mara baada ya kushiriki kupiga Kura katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi kwenye ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Dodoma Makulu, Mtaa wa Msangalale jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (wa kwanza kushoto) akipokea fomu ya kushiriki kupiga Kura kutoka kwa Wasimamizi wa Uchaguzi katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa wa Mwatano jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akionesha kidole kilichopakwa wino mara baada ya kushiriki kupiga Kura katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi kwenye ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa wa Mwatano jijini Dodoma.

 



Monday, October 27, 2025

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAWAPONGEZA WASTAAFU WA OFISI HIYO KWA KULITUMIKIA TAIFA KIKAMILIFU

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 28 Oktoba, 2025

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imewapongeza Watumishi wa Ofisi hiyo waliofikia ukomo katika Utumishi wa Umma kutokana na utumishi uliotukuka kwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ambao umechangia kutolewa kwa huduma bora katika Idara walizokuwa wakifanyia kazi.

Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, leo tarehe 27 Oktoba, 2025, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, SACP. Ibrahim Mahumi amesema kufikisha umri wa miaka 60 sio mchezo, ni jambo la kumshukuru Mungu.

 “Hongereni sana, mmeondoka katika Utumishi wa Umma mkiwa na sifa nzuri katika kulitumikia taifa na mkiwa na afya njema ni mfano mzuri wa kuigwa na tunaoendelea kufanya kazi,” amesema SACP. Mahumi.

SACP. Mahumi amemshukuru Katibu Mkuu-UTUMISHI kupitia Idara ya Utawala kwa kuanzisha utamaduni wa kukutana kila Jumatatu na kuwa na ubunifu mbalimbali wa kuwaweka watumishi pamoja kwa lengo la kuboresha utendaji.

“Tangu jambo hili la kukutana pamoja kila siku ya Jumatatu kupata elimu ya kuboresha utendaji kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kiutendaji, nawasihi tuendelee kuyatumia mafunzo haya kuboresha utendaji zaidi.” Amesisitiza.

Akitoa neno la shukrani, Mtumishi Mstaafu wa Ofisi hiyo, Bw. Jerome Nchimbi amesema, ndani ya miaka 8 aliyofanya kazi katika ofisi hiyo amejfunza masuala mengi ya Kiutumishi pamoja na kufundishwa upendo, ushirikiano na kuwajali watu.

Kwa upande wake, Mstaafu mwingine, Bi. Godliver Byemerwa ametoa wito kwa Watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kuwahudumia Wananchi kwa moyo wa upendo na ufanisi mkubwa kwa kuwa ofisi hiyo ni kioo cha jamii.

Aidha, Ofisi hiyo imewapongeza Watumishi waliozaliwa mwezi Oktoba na kuwatakia heri katika maisha yao ya Utumishi wa Umma ili kuwatumikia wananchi pamoja na kuongeza tija katika utendajikazi.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi (wakwanza kulia) akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa Watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa ofisi hiyo, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. 


Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakiwasikiliza Watumishi wastaafu Bw. Jerome Nchimbi na Bi. Godliver Byemerwa (hawapo pichani) wa ofisi hiyo walipokuwa wakitoa shukrani kwa Viongozi na Watumishi mara baada ya kufikia ukomo katika Utumishi wa Umma. 


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifurahia jambo wakati Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa ofisi hiyo, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa Watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. 

Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa Watumishi hao katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. 

Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa ofisi hiyo, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, wa ofisi hiyo, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Mtumishi Mstaafu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Jerome Nchimbi akitoa neno la shukrani kwa Wakurugenzi na Watumishi wa ofisi hiyo baada ya kuhitimisha Utumishi wake wa Umma.

Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa ofisi hiyo, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. 

Mtumishi Mstaafu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Godliver Byemerwa akitoa neno la shukrani kwa Wakurugenzi na Watumishi wa ofisi hiyo baada ya kuhitimisha Utumishi wake wa Umma.

Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa ofisi hiyo, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.