Thursday, December 11, 2025

MHE. RIDHIWANI KIKWETE AWAKUMBUSHA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA KUZINGATIA WAJIBU WAO WA KUSIMAMIA MAADILI BILA UPENDELEO

 Na Antonia Mbwambo na Eric Amani-Dodoma

Tarehe 11 Disemba, 2025

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, ametoa wito kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa weledi, uadilifu na bila upendeleo kwa kiongozi yeyote.

Akizungumza wakati akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Nchemba kwa ajili ya kuzungumza na watendaji wa Sekretarieti hiyo, Mhe. Kikwete amesisitiza umuhimu wa chombo hicho katika kusimamia maadili kwa kuzingatia misingi ya sheria, uwazi, ukweli na usawa, ili kuendelea kujenga taswira njema ya utumishi wa umma nchini.

Ameeleza kuwa viongozi wa umma wana wajibu mkubwa kwa jamii, hivyo ni muhimu Sekretarieti hiyo kutekeleza dhima yake ya kisheria ya kuhakikisha viongozi wote wanazingatia miiko na maadili katika kutekeleza majukumu yao.

“Hatuwezi kuwa na Serikali ambayo viongozi wanalalamikiwa kwamba ni wapotofu wa Maadili na sisi kama chombo cha kusimamia Maadili ya Viongozi wa Umma tumekaa kimya” Waziri Kikwete alisema.

Aidha, ametoa rai kwa watumishi wa Sekretarieti ya Maadili kuimarisha ushirikiano, kuendesha uchunguzi kwa haki bila upendeleo na kutoa elimu ya kutosha kuhusu maadili kwa viongozi wa umma na wananchi kwa ujumla.

Kwa upande wao, watendaji wa Sekretarieti hiyo wamemhakikishia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – UTUMISHI Mhe. Ridhiwani Kikwete kuwa wataendelea kufanya kazi kwa kuzingatia uwajibikaji, uadilifu na weledi ili kuimarisha imani ya wananchi katika mifumo ya utawala bora


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mwigulu Nchemba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na menejimenti na watumishi wa Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakati wa ziara yake ya  kikazi aliyoifanya katika Ofisi hiyo leo tarehe Disemba 11, 2025 Jijini Dodoma. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete na Kushoto ni Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Sekretarieti ya Maadili Jaji Sivangilwa Mwangesi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na Katibu Mkuu Ikulu Bw. Mululi Mahendeka wakati wakimsubiria Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Mwigulu Nchemba awasili katika Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambapo alikuwa na ziara ya kikazi leo Disemba 11, 2025 jijini Dodoma.

Waziri Mkuu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Mwigulu Nchemba (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) baada ya kuwasili katika Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambapo alikuwa na ziara ya kikazi leo Disemba 11, 2025.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna wa Maadili,Jaji Mstaafu Bw. Sivangilwa Mwangesi (katikati) pamoja na Katibu Mkuu Ikulu Bw. Mululi Mahendeka (kulia) wakati wakimsubiria Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kuwasili katika Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa ziara ya kikazi iliyofanyika leo Disemba 11, 2025 jijini Dodoma.

1.  Waziri Mkuu  wa Jamhurin ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Mwigulu Nchemba akiwasili katika Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambapo alikuwa na ziara ya kikazi leo Disemba 11, 2025

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mwigulu Nchemba akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambapo alikuwa na ziara ya kikazi leo Disemba 11, 2025 jijini Dodoma.Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete,wengine ni Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Sekretarieti ya Maadili Jaji Sivangilwa Mwangesi (wa tatu kulia) na Katibu Mkuu Ikulu Bw. Mululi Mahendeka (wa kwanza kushoto).


Menejimenti na Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili wakimsikiliza Waziri Mkuu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Mwigulu Nchemba (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi hiyo leo Disemba 11, 2025 jijini Dodoma.


Menejimenti na Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili wakimsikiliza Waziri Mkuu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Mwigulu Nchemba (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi hiyo leo Disemba 11, 2025 jijini Dodoma.

9(


No comments:

Post a Comment