Na. Mwandishi Wetu-Dar es Salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ameipongeza
Bodi, Menejimenti na Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) kwa kuongoza
na kusimamia Ndege za Serikali kwa weledi na ufanisi mkubwa.
Waziri Kikwete amesema hayo Desemba 12, 2025 jijini Dar es salaam
wakati alipotembelea ofisi ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) kwa lengo la
kujitambulisha.
“Ninaipongeza Bodi kwa kuendelea kuwa washauri wazuri na kufanya uendelevu wa
Wakala, binafsi ninaridhika na utendaji kazi wake. Pia Nitumie fursa hii
kuwapongeza watumishi wote kwa ustadi wenu mkubwa wa kusimamia Ndege za
Serikali, mimi na Naibu Waziri wa ofisi yangu Mhe. Regina Qwaray
tunawahakikishia ushirikiano wa dhati wakati wote wa uongozi wetu” alisema Mhe.
Kikwete.
Aidha,
Mhe. Kikwete amewapongeza kwa kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi ambao
unaonekana kuridhisha viongozi wanawahudumia. Hivyo, ametoa rai pia kwa
watumishi hao kumpa ushirikiano Naibu Waziri Mhe. Regina Qwaray kwa kuwa
anamfahamu uwezo wake katika kazi na atasaidia kuongeza ufanisi mara dufu.
Vile
vile Mhe. Kikwete amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumpa nafasi ya kuongoza Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo TGFA ni moja ya
taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo.
Naye,
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray
ameahidi kutoa ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya taasisi hiyo muhimu
katika Taifa.
“Leo tumekuja kujitambulisha ili tupate kufahamiana kwa kuwa sisi ndio tutafanya kazi pamoja, naomba tuendelee kuwa na ari ile ile ya kufanya kazi kwa ushirikiano ili tuweze kufanikiwa” alisema Mhe. Qwaray.
Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Ndege za Serikali Capt. Budodi
Nicholaus Budodi alisema kuwa Wakala inaendelea vizuri kusimamia miradi
mbalimbali inayoendelea katika ofisi hiyo.
Vile vile, kwa niaba ya taasisi ameahidi kuendelea kuwa wasikivu katika maelekezo wanapata kutoka kwa viongozi na kutekeleza kwa wakati na kwa ufanisi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Menejimenti na
Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) wakati alipotembelea
ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Wakala ya Ndege za
Serikali (TGFA), Capt. Budodi Budodi (aliyesimama) akisoma taarifa ya taasisi hiyo pamoja na
maendeleo ya ujenzi wa Karakana ya Wakala ya Ndege za Serikali wakati Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete alipotembelea taasisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali
(TGFA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati
Waziri huyo alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali, Prof. Mhandisi Idrissa
Mshoro
(kushoto) akifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati Waziri
huyo alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
(wapili kutoka kushoto) akielekea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Karakana ya Wakala wa Ndege za
Serikali jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Naibu
Waziri wa Ofisi yake Mhe. Regina Qwaray. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Wakala ya Ndege za
Serikali (TGFA), Capt. Budodi
Budodi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wakwanza kushoto)
akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA), Capt. Budodi Budodi (wakwanza kulia). Wa pili kutoka kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Regina
Qwaray na wa pili kutoka kushoto
ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za
Serikali, Prof. Mhandisi Idrissa Mshoro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia)
akifurahia jambo kabla ya kuzungumza na Menejimenti na Watumishi wa Wakala ya
Ndege za Serikali (TGFA) wakati alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni
Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Regina Qwaray.
Mkurugenzi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA), Capt. Budodi Budodi (wakwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wapili kutoka kushoto). Wa pili kutoka kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia)
akiwasili katika ofisi ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) wakati alipotembelea
ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akiwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Ofisi ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) kabla ya kuzungumza na Menejimenti na Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) wakati alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Regina Qwaray.
Sehemu ya Menejimenti ya Wakala ya Ndege za Serikali
(TGFA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati Waziri
huyo alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali
(TGFA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati
Waziri huyo alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina
Qwaray (wa kwanza kulia) akisalimiana na Mwenyekiti
wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali, Prof. Mhandisi Idrissa
Mshoro. Katikati ni Mkurugenzi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA), Capt. Budodi Budodi.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete akisalimiana na Viongozi, Watendaji na Watumishi
wa Wakala ya
Ndege za Serikali baada ya kuwasili katika ofisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja
na Watumishi na Menejimenti ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) baada ya
kuzungumza nao alipokwenda kujitambulisha katika ofisi hiyo jijini Dar es
Salaam

No comments:
Post a Comment