Na Veonica Mwafisi-Dar es Salaam
Tarehe 12 Disemba, 2025
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali kupitia Ofisi yake inaonesha dhamira
thabiti ya kujenga Utumishi wa Umma wenye ufanisi, uwajibikaji na unaozingatia
misingi ya utawala bora ili kwenda sambamba na matarajio ya Dira ya Maendeleo
ya Taifa ya 2050.
Waziri Kikwete amesema hayo wakati wa Mkutano wake na
Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es
salaam Desemba 12, 2025. Mkutano huo ulilenga kutoa taarifa ya namna Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inavyotekeleza wajibu
wake kwa Taasisi za umma, Watumishi wa Umma na Wananchi kwa jumla.
Mhe. Kikwete ameongeza kuwa, dhamira hiyo imeweka
vipaumbele ambavyo ni kuongeza fursa za ajira na ustawi wa vijana wa
kitanzania, maboresho ya mifumo ya ajira, utoaji wa huduma, mafunzo ya kujenga
uwezo, usimamizi wa rasilimaliwatu pamoja na kuimarisha mifumo ya mawasiliano kati
ya Serikali na wananchi.
Mhe. Kikwete alibainisha kuwa Serikali inaendelea
kuhakikisha nafasi za ajira katika Utumishi wa Umma zinakuwa za wazi na
ushindani kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ili
kuwajengea Watanzania imani na uaminifu kwa Serikali yao kwa ustawi wa Taifa.
Vile vile, Mhe. Kikwete amesema, kupitia Dira ya Taifa ya
Maendeleo 2050 imeelekeza Sekta ya kipaumbele iwe na uwezo wa kuzalisha ajira
na kuongeza fursa ya ajira kwa vijana, kuongeza kipato kwa wananchi na
kupunguza umaskini kwa kuzingatia viwango vya juu vya weledi unaopatikana na
kufuata misingi ya haki, umahiri na utendaji bora.
Aidha, Mhe. Kikwete ameongeza kuwa, katika kufanikisha
maelekezo ya Dira 2050, kupitia Serikali kwa mwaka wa Fedha 2025/26 kibali cha
nafasi 41,500 za ajira zikiwemo nafasi 12,000 za ajira ambazo ni ahadi ya Mhe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoahidi kutoa nafasi 5,000 za kada
za Afya na nafasi 7,000 za Walimu wa Masomo ya Sayansi na Hisabati ambazo ni
uzalishaji wa ajira zilizo rasmi ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani.
Mhe. Kikwete amesema kuwa, ili kuhakikisha usaili
unafanyika kwa wakati na kwa lengo la kuongeza ufanisi, usaili wa mchujo wa
nafasi hizo utafanyika kwa kutumia mfumo wa kieletroniki uitwao “Online
Aptitude Test (OATS)” na utafanyika katika vituo mbalimbali kama vile Taasisi
za Elimu ya Juu, Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi na Ufundi Stadi (VETA) na Shule za
Sekondari zenye maabara za Komputa zinazopatikana katika mikoa yote na Vituo
mahsusi kwa Unguja na Pemba.
“Mhe. Rais Dkt. Samia aliahidi baada ya kuingia madarakani
atatoa nafasi 5,000 za kada za Afya na nafasi 7,000 za Walimu ndani ya siku 100
na tayari nafasi za ajira 12,000 zimeshatangazwa na waombaji wenye sifa
wameitwa kwenye usaili utakaofanyika kuanzia tarehe 13 Desemba, 2025 katika
mikoa yote Tanzania Bara na Vituo mahsusi kwa Unguja na Pemba,” Amefafanua Mhe.
Kikwete.
Pia, Waziri huyo aliwaomba wandishi wa habari kuendelea
kuwahabarisha na kuwaelimisha Watanzania hususan vijana, kutambua fursa
zilizopo na kuzitumia kwa manufaa ya taifa. Utambuzi huo unaifanya Serikali kuendelea
na jitihada zake za kukuza ujuzi, kuhimiza maadili, kupanua fursa za makazi
bora na kuandaa vijana wa Kitanzania ili kukabiliana na uchumi wa kidijiti.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Waandishi
wa Habari (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wake na Waandishi hao
uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es salaam uliolenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi
yake.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo kwenye Mkutano
wake na Waandishi hao uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es
salaam. Wa kwanza kulia waliokaa ni Naibu Waziri, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Regina Qwaray. Wengine ni
Viongozi na Watendaji wa Ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wanne kutoka kushoto) akimsikiliza, Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo, Bi. Zamaradi Kawawa (hayupo pichani) alipokuwa
akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri huyo kuzungumza na
Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI. Watatu
kutoka kushoto ni Naibu Waziri, wa Ofisi
yake Mhe. Regina
Qwaray na wengine ni Viongozi na Watendaji wa Ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ofisi yake Mhe. Regina Qwaray (kushoto) kabla ya kuanza kwa
Mkutano wa Waziri huyo na Waandishi wa
Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es salaam kwa
lengo la kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake.
Mwandishi wa Habari kutoka Kituo cha Habari Azam Tv, Bi. Sheila Mkumba
(aliyeshika kipaza sauti) akiuliza swali kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo
pichani) wakati wa Mkutano wa Waziri huyo na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo
jijini Dar es salaam kwa lengo la kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya
ofisi yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiwa na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira
katika Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (kulia) kabla ya Waziri huyo
kuzungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Mkutano wake na Waandishi hao uliofanyika katika Ukumbi wa Habari
Maelezo jijini Dar es salaam uliolenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu
ya ofisi yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyesimama kulia) akizungumza na Waandishi wa
Habari wakati wa Mkutano wake na Waandishi hao
uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es salaam uliolenga
kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake. Wa pili kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa
Ofisi yake Mhe. Regina Qwaray. Wengine ni Viongozi na Watendaji wa Ofisi hiyo.
Mwandishi wa Habari kutoka Kituo cha Habari Radio Maria, Bw. Martin Joseph
(aliyeshika kipaza sauti) akiuliza swali kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo
pichani) wakati wa Mkutano wa Waziri huyo na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo
jijini Dar es salaam kwa lengo la kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya
ofisi yake.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo kwenye Mkutano
wake na Waandishi hao uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es
salaam. Wengine ni Viongozi na Watendaji wa Ofisi yake.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Regina Qwaray (watatu kutoka
kushoto) akifuatilia Mkutano wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es salaam
uliolenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake.


No comments:
Post a Comment