Monday, April 30, 2018

Wednesday, April 18, 2018

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAPATA MFANYAKAZI BORA WA MWAKA 2018


Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Dorothy Mwaluko akifungua mkutano wa kumchagua mfanyakazi bora wa mwaka 2018 wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora uliofanyika mapema leo katika ofisi hiyo mkoani Dodoma.

Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Dorothy Mwaluko akitoa maelekezo kuhusu uchaguzi wa kumpata mfanyakazi bora wa ofisi wa mwaka 2018.

Wawakilishi wa wafanyakazi bora wa Idara/Vitengo vya Ofisi ya Rais-Utumishi wakishuhudia zoezi la kuhesabu kura ili kumpata mfanyakazi bora wa ofisi wa mwaka 2018.

Tuesday, April 17, 2018

WATUMISHI WA UMMA 4,812 KUNUFAIKA NA MAFUNZO NCHINI CHINA C


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ukumbi wa Idara ya Habari - Bunge kuhusu Watumishi wa Umma 4,812 kunufaika na fursa 659 za mafunzo ya muda mfupi na mrefu zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaka 2018.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro  akifafanua jambo kuhusu  Watumishi wa Umma 4,812 watakaonufaika na fursa 659 za mafunzo ya muda mfupi na mrefu zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaka 2018.

Monday, April 16, 2018

MHE. MKUCHIKA AWAELEKEZA WAAJIRI SERIKALINI KUTOKWAMISHA UHAMISHO WA WATUMISHI WA UMMAWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu.)  Mhe. George Mkuchika (Mb) akijibu hoja za wabunge wakati akihitimisha Hotuba ya Bajeti ya Ofisi yake kwa Mwaka wa Fedha 2018/19.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likijadili hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2018/19 iliyowasilishwa Bungeni  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mstaafu.)  Mhe. George Mkuchika (Mb).

Thursday, April 12, 2018

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA, MHE. KAPT (MST) GEORGE H. MKUCHIKA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2018/19 YA OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA NA TAASISI ZAKE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2018/19 ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora na Taasisi zake.