Wednesday, November 27, 2019

UTUMISHI YASHIRIKI UZINDUZI WA KAMPENI YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA, JIJINI DODOMA


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika kitaifa  tarehe 26/11/2019 kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizindua Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Wednesday, November 20, 2019

KAMISHNA WA TUME YA MAADILI NA KUZUIA RUSHWA NCHINI KENYA ATEMBELEA OFISI YA RAIS UTUMISHI

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ACP Ibrahim Mahumi akimkabidhi Miongozo mbalimbali ya Mapambano dhidi ya Rushwa Kamishna wa Tume ya Maadili na Kuzuia Rushwa nchini Kenya, Bibi Rose Mghoi Machaira baada ya kikao kilichofanyika tarehe 18/11/2019 Ofisi ya Rais Utumishi, Mtumba, jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ACP Ibrahim Mahumi akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna wa Tume ya Maadili na Kuzuia Rushwa nchini Kenya, Bibi Rose Mghoi Machaira mara baada ya kikao kilichofanyika tarehe 18/11/2019 Ofisi ya Rais Utumishi, Mtumba, jijini Dodoma. Wengine ni Watendaji kutoka Ofisi ya Rais, Utumishi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Tume ya Maadili na Kuzuia Rushwa-Kenya.


Tuesday, November 19, 2019

MIAKA MINNE YA MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KATIKA ENEO LA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA


MAWAZIRI WENYE DHAMANA YA UTUMISHI NA UTAWALA BORA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR WAKUTANA KUZUNGUMZIA NAMNA YA KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA KWA UMMA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifungua kikao kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha muungano kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (mbele) wakiwa kwenye kikao kazi na baadhi ya watendaji wa Serikali ya Muungano kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kikao kazi hicho kilikuwa na lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha muungano.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha muungano, kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Waziri huyo ndiye mwenye dhamana ya kushughulikia masuala ya muungano.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Haroun Ali Suleiman wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akizungumza katika kikao kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha Muungano kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Friday, November 15, 2019

WATUMISHI 44,800 WA KADA YA AFYA KUAJIRIWA NCHINI KWA MWAKA WA FEDHA 2019/20 ILI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Silafu Jumbe Maufi  Bungeni leo jijini Dodoma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililohusu  mpango wa Serikali kuajiri watumishi wa kada ya afya ili kuboresha huduma za afya nchini.


Thursday, November 14, 2019

TAASISI ZA UMMA NCHINI ZATAKIWA KUWAPATIA HUDUMA YA USAFIRI WATUMISHI WA UMMA WENYE ULEMAVU


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Amina S. Mollel  Bungeni leo jijini Dodoma, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililohusu  mpango  wa Serikali wa kuwapatia huduma ya usafiri Watumishi wa Umma wenye Ulemavu.


Tuesday, November 12, 2019

TASAF YAPONGEZWA NA KAMATI YA BUNGE KWA MAFANIKIO YA MALIPO YA RUZUKU KIELEKRONIKI KWA KAYA MASKINI


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Jasson Rweikiza (Mb) akifungua kikao kazi cha kamati yake na viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye lengo la kupokea mrejesho wa matumizi ya TEHAMA katika shughuli zinazofanya na TASAF uliowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma jana.


Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wakifuatilia mada kuhusu matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma jana. 
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Rehema Migilla (Mb) akichangia hoja kuhusu mada ya matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma jana.


Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga akitoa ufafanuzi wa hoja zilizowasilshwa na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Mwanne Mchemba (Mb) akifunga kikao kazi cha kamati yake na viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye lengo la kupokea mrejesho wa matumizi ya TEHAMA katika shughuli zinazofanya na TASAF uliowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma jana.

Saturday, November 9, 2019

TAASISI YA UONGOZI YATAKIWA KUTOA MAFUNZO KWA VIONGOZI KATIKA MAENEO YAO YA KAZI ILI KUIMARISHA UTAWALA BORA



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akihimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Taasisi ya Uongozi (UONGOZI Institute) ( hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana.

Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Uongozi (UONGOZI Institute) wakisikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha watumishi hao na Naibu waziri huyo chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika katika ukumbi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya Uongozi (UONGOZI Institute) mara baada ya kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana.



Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof. Joseph Semboja akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) mara baada ya Naibu Waziri huyo kuwasili katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kikao kazi cha kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hiyo.