Tuesday, November 12, 2019

TASAF YAPONGEZWA NA KAMATI YA BUNGE KWA MAFANIKIO YA MALIPO YA RUZUKU KIELEKRONIKI KWA KAYA MASKINI


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Jasson Rweikiza (Mb) akifungua kikao kazi cha kamati yake na viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye lengo la kupokea mrejesho wa matumizi ya TEHAMA katika shughuli zinazofanya na TASAF uliowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma jana.


Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wakifuatilia mada kuhusu matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma jana. 
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Rehema Migilla (Mb) akichangia hoja kuhusu mada ya matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma jana.


Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga akitoa ufafanuzi wa hoja zilizowasilshwa na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Mwanne Mchemba (Mb) akifunga kikao kazi cha kamati yake na viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye lengo la kupokea mrejesho wa matumizi ya TEHAMA katika shughuli zinazofanya na TASAF uliowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma jana.

No comments:

Post a Comment