Saturday, November 2, 2019

TAKUKURU NA POLISI WAASWA KUFANYIA KAZI TAARIFA ZA RUSHWA ZINAZOTOLEWA NA WANANCHI ILI WAENDELEE KUTOA TAARIFA HIZO



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na wananchi na wadau (Hawapo pichani) waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni ya UTATU ya kupambana na rushwa ya barabarani  inayohusisha TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Wadau mbalimbali, uliofanyika jana katika  Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wananchi na wadau waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni ya UTATU ya kupambana na rushwa ya barabarani inayohusisha TAKUKURU na Jeshi la Polisi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Hayupo pichani) kabala ya waziri huyo kuzindua ramsi kampeni hiyo jana katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akikata utepe kuzindua rasmi Kampeni ya UTATU ya kupambana na rushwa ya barabarani  inayohusisha TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Wadau mbalimbali, uzinduzi  huo uliofanyika jana  katika  Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akitoa neno la utangulizi kuhusu uzinduzi wa Kampeni ya UTATU ya kupambana na rushwa ya barabarani kabla ya kumaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) kuzindua rasmi kampeni hiyo kwa niaba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana.

Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akizungumza kuhusu uzinduzi wa Kampeni ya UTATU ya kupambana na rushwa ya barabarani inayohusisha TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Wadau mbalimbali, uliofanyika jana katika  Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kuzuia Rushwa wa TAKUKURU Bi. Sabina Seja akizungumza kwa niaba Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuhusu uzinduzi wa Kampeni ya UTATU ya kupambana na rushwa ya barabarani inayohusisha TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Wadau mbalimbali ulifanyika jana katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana.









No comments:

Post a Comment