Wednesday, December 31, 2014

Monday, December 15, 2014

WATAALAMU 12 WA KUJITOLEA KUTOKA NCHINI JAPANI WAMALIZA MUDA WA KUTOA HUDUMA NCHINI

Mtalaamu wa kujitolea Bw.Keisuke Yamamoto akitoa mada wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalamu wa kujitolea kutoka Japani iliyofanyika Utumishi.

Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.Mick Kiliba (kushoto) akimpongeza mmoja kati ya watalaam wa kujitolea kutoka nchini Japani Bw.Keisuke Yamamoto baada ya kumaliza muda wa kujitolea nchini.

Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw. Mick Kiliba (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa kujitolea kutoka nchini Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini mara baada ya hafla fupi iliyofanyika Utumishi.Wengine ni Maafisa Waandamizi kutoka Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Thursday, December 11, 2014

Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji  Maadili ya Ofisi ya Rais - Utumishi Bw. Mathew Kirama akitoa maoni katika kikao cha kujadili matokeo ya utafiti juu ya hali ya maadili katika Utumishi wa Umma.

Mtaalamu mwelekezi toka Chuo Kikuu cha Mzumbe Dkt. Francis Mwaijande (wa pili toka kushoto) akiwasilisha matokeo ya utafiti juu ya hali ya uzingatiaji wa maadili katika Utumishi wa Umma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Utumishi Bw. HAB Mkwizu (wa kwanza kulia) akizungumza katika kikao cha kujadili matokeo ya utafiti juu ya hali ya uzingatiaji wa maadili katika Utumishi wa Umma.

Mwakilishi wa shirika lisilo la kiserikali la TWAWEZA Bw. Joseph Mbando (aliyesimama) akitoa maoni katika kikao cha kujadili matokeo ya utafiti juu ya hali ya uzingatiaji maadili katika Utumishi wa Umma.