Thursday, June 25, 2015

UTUMISHI YAWAAGA WATAALAM 12 WA KUJITOLEA KUTOKA JAPANI WALIOMALIZA MUDA WA KUTOA HUDUMA NCHINI


Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bi.Sekiko Masui aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini  katika hafla ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi leo.


Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi Bw.HAB Mkwizu ( wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa Kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini baada ya hafla ya kuwaaga iliyofanyika ofisini kwake leo. Wengine ni baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. 

Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bi. Haruka Ota akielezea namna alivyofanya kazi katika Maktaba Kuu ya Taifa,wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi leo.  

Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bw.Koji Ueda akielezea namna alivyofanya kazi katika shule ya Sekondari Sogesca iliyoko mkoani Mwanza,katika hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi leo.


Wataalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Utumishi Bw.HAB Mkwizu katika hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika ukumbi wa Utumishi leo.

Wednesday, June 24, 2015

KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2015 CHAFANA

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akihutubia wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2015 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana.

Moja kati ya washindi wa tuzo za Wiki ya Utumishi wa Umma 2015 wakifurahia tuzo waliyoipata wakati wa kilele za Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2015 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana.

Baadhi ya Watumishi wa Umma na wananchi waliohudhuria kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2015 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakimsikiliza mgeni rasmi Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mh. Ali Hassan Mwinyi (hayupo pichani) jana.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mh. Ali Hassan Mwinyi  (wa pili kutoka kushoto) akitembelea mabanda katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2015  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana. Anayemuongoza ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. HAB Mkwizu (watatu kutoka kushoto).

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mh. Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akimkabidhi tuzo mmoja wa wawakilishi wa taasisi zilizopata tuzo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2015 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana.

Tuzo zilizokabidhiwa Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma jana tarehe 23 Juni, 2015.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mh. Ali Hassan Mwinyi  (wa pili kutoka kushoto) akitembelea mabanda katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2015  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana. Anayemuongoza ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. HAB Mkwizu (watatu kutoka kushoto).

Saturday, June 20, 2015

OFISI YA RAIS UTUMISHI YAMUAGA RASMI KATIBU MKUU MSTAAFU BW.GEORGE D. YAMBESI

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga  Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. George D. Yambesi (wa pili kutoka kushoto) iliyofanyika Leaders Club. Wengine ni Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utumishi Bi.Celina O. Kombani (Mb) (wa pili kutoka kulia) na Mama Yambesi  (kushoto).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utumishi Mhe. Celina O. Kombani (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga  Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. George D. Yambesi (hayupo pichani) iliyofanyika Leaders Club. Kushoto kwake ni Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi.
Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Rais - Utumishi Bw. George D. Yambesi (aliyesimama)  akizungumza katika hafla ya kuagwa iliyofanyika viwanja vya Leaders Club
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utumishi Mhe. Celina O. Kombani (Mb)(kulia) akimkaribisha Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Rais - Utumishi Bw. George D. Yambesi katika hafla ya kumuaga iliyofanyika viwanja vya Leaders Club. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utumishi Mhe. Celina O. Kombani (wa pili kutoka kulia) akipokea kombe la mshindi wa kwanza wa mpira wa pete la mashindano ya Mei Mosi 2015 kutoka kwa Kapteni wa Timu ya Netiboli ya utumishi Bi. Elizabeth Fusi katika viwanja vya Leaders Club. Wanaoshuhudia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) ,Katibu Mkuu Mstaafu Bw. George D. Yambesi (wa pili kutoka kushoto) na Mama Yambesi (kushoto).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utumishi Mhe. Celina O. Kombani (Mb) (wa pili kutoka kulia) akionyesha Tuzo ya Ununuzi Bora wa Umma  ya Ofisi ya Rais - Utumishi iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) hivi karibuni baada ya kushinda.Wanaoshuhudia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) ,Katibu Mkuu Mstaafu Bw. George D. Yambesi (wa pili kutoka kushoto) na Mama Yambesi (kushoto).
Baadhi ya watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais-Utumishi wakiwa katika hafla ya kumuaga Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. George D. Yambesi iliyofanyika Leaders Club.Wednesday, June 17, 2015

BALOZI SEFUE AFUNGUA RASMI KONGAMANO LA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akifungua Kongamano la Wiki ya Utumishi wa Umma katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Dr. Matern Lumbanga akitoa Mada kuu ya utangulizi katika Kongamano la Wiki ya Utumishi wa Umma.
Mwenyekiti wa Kongamano, Katibu Mkuu Mstaafu Bw. George D. Yambesi, akitoa maelekezo kuhusu mada zilizowasilishwa wakati akiongoza kongamano la Wiki ya Utumishi wa Umma 2015.
Kaimu Katibu Mkuu-Utumishi Bw. HAB Mkwizu akitoa neno la shukrani baada ya ufunguzi wa Kongamano la Wiki ya Utumishi wa Umma.
Sehemu ya washiriki wa Kongamano wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue (hayupo pichani), kushoto ni Katibu Mstaafu Tume ya Utumishi Bi. Thecla Shangali, akifuatiwa na Katibu Mkuu Mstaafu-Ikulu Bi. Rose Lugembe.
Sehemu ya washiriki vijana "Young Professional" wakisikiliza maelekezo wakati wa Kongamano la Wiki ya Utumishi wa Umma. 

Tuesday, June 16, 2015

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2015 YAFUNGULIWA RASMI

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.HAB Mkwizu akifungua rasmi Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.HAB Mkwizu (hayupo pichani) katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Wakurugenzi na Watendaji Wakuu kutoka taasisi mbalimbali za Umma wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.HAB Mkwizu alipokuwa akifungua rasmi Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.HAB Mkwizu akisaini kitabu cha wageni alipotembelea  banda la Wakala ya Serikali Mtandao-eGA kabla ya kufungua rasmi Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi  na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.Mick Kiliba akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.HAB Mkwizu (hayupo pichani) kufungua rasmi Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.HAB Mkwizu (hayupo pichani) katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Thursday, June 11, 2015

MKUTANO WA PILI WA BARAZA KUU LA TATU LA WAFANYAKAZI KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Pili wa Baraza Kuu la Tatu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma wakiwa katika mkutano huo ulifanyika mjini Dodoma katika Ukumbi wa St. Gaspar Hotel.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akifungua Mkutano wa Pili wa Baraza Kuu la Tatu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma mjini Dodoma katika Ukumbi wa St. Gaspar Hotel.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akizungumza wakati akifungua  Mkutano wa Pili wa Baraza Kuu la Tatu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma mjini Dodoma katika Ukumbi wa St. Gaspar Hotel. Kulia kwake ni baadhi ya waandishi wa habari wakifutilia hotuba yake kwa umakini.


Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Mathias B. Kabunduguru akizungumza katika Mkutano wa Pili wa Baraza Kuu la Tatu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma mjini Dodoma katika Ukumbi wa St. Gaspar Hotel.


Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) kufungua Mkutano wa Pili wa Baraza Kuu la Tatu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma mjini Dodoma katika Ukumbi wa St. Gaspar Hotel.