Thursday, June 25, 2015

UTUMISHI YAWAAGA WATAALAM 12 WA KUJITOLEA KUTOKA JAPANI WALIOMALIZA MUDA WA KUTOA HUDUMA NCHINI


Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bi.Sekiko Masui aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini  katika hafla ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi leo.


Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi Bw.HAB Mkwizu ( wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa Kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini baada ya hafla ya kuwaaga iliyofanyika ofisini kwake leo. Wengine ni baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. 

Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bi. Haruka Ota akielezea namna alivyofanya kazi katika Maktaba Kuu ya Taifa,wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi leo.  

Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bw.Koji Ueda akielezea namna alivyofanya kazi katika shule ya Sekondari Sogesca iliyoko mkoani Mwanza,katika hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi leo.


Wataalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Utumishi Bw.HAB Mkwizu katika hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika ukumbi wa Utumishi leo.

No comments:

Post a Comment