Monday, August 26, 2019

MRADI WA KUFUA UMEME WA MAJI WA JULIUS NYERERE KATIKA MAPOROMOKO YA MTO RUFIJI UNAOTEKELEZWA NA SERIKALI ULIASISIWA NA BABA WA TAIFA MWAKA 1975



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisoma kitabu cha Tanzania News Review kinachoonyesha kuwa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere katika Maporomoko ya Mto Rufiji unaojulikana kama Julius Nyerere HydroPower Project uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere mnamo mwaka 1975.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia baadhi ya nyaraka muhimu zinazotunzwa na Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati wa ziara yake ya kikazi katika Idara hiyo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia baadhi ya nyaraka za Waasisi wa Taifa zilizotunzwa katika maktaba ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi katika Idara hiyo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza uhifadhi mzuri wa nyaraka alipotembelea maktaba ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dar es Salaam na kushuhudia baadhi ya watafiti wakipata huduma ya taarifa zitakazowawezesha kukamilisha tafiti zao.

No comments:

Post a Comment