Na Antonia Mbwambo-Dodoma
Tarehe 24 Novemba, 2025
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amefanya ziara ya kikazi Tume ya Utumishi wa umma na kutoa maelekezo mbalimbali ya kuboresha utendaji kwa ustawi wa taifa.
Mhe.
Kikwete ametoa maelekezo hayo akiwa kwenye ziara yake ya kwanza katika Tume
hiyo tangu alipoapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan tarehe 18 Novemba, 2025 kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Pamoja na
masuala mengine, Mhe. Kikwete ameilekeza Tume hiyo kuendelea kutenda haki
katika kushughulikia Rufani na malalamiko ya Watumishi wa Umma na Mamlaka za
Nidhamu. “Tutende
haki, tusimame katika haki, lazima tuangalie katika utoaji haki, taratibu
zizingatiwe, uchunguzi wa kina ufanyike kabla ya kumchukulia mtumishi hatua,”
amesisitiza Mhe. Kikwete.
Mhe.
Kikwete ameisisitiza Tume kuendelea kutoa Miongozo ya masuala ya Ajira na
Nidhamu ambayo husaidia kuwa na tafsiri sahihi ya utekelezaji wa sheria katika
Utumishi wa Umma.
Aidha, ameielekeza
Tume hiyo kuendelea kufanya ukaguzi wa masuala ya Rasilimaliwatu na uzingatiaji
wa Sheria katika Taasisi za Umma hususani kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa
na Mashirika ya Umma ili kuhakikisha Watumishi wa Umma wanapata haki zao
kuanzia wanapoajiriwa hadi wanapostaafu.
Mhe.
Kikwete ametoa wito kwa Tume hiyo kuwashauri waajiri kuweka mazingira wezeshi
ya kufanya kazi (vitendea kazi, maslahi na miundo mbinu sahihi ya kufanya kazi)
na kuhakikisha uwepo wa Mabaraza ya Wafanyakazi yaliyo hai na yanafanya kazi
kwa mujibu wa Sheria.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi akitaka ufafanuzi wa jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Ridhiwani Kikwete katika Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma leo tarehe 24 November,2025 Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa tatu kulia) Kikwete akiwa
katika picha ya pamoja na Menejimenti Ofisi ya Tume ya Utumishi
wa Umma wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi
hiyo leo
tarehe 24. Novemba, 2025 jijini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Waziri
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina
Qwaray na Kushoto kwake ni Kaimu Katibu wa Tume ya
Utumishi wa Umma Bw. John Mbisso.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akimsikiliza Waziri wa Ofisi hiyo Mh. Ridhiwani Kikwete (hayupo
pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi hiyo leo tarehe 24. Novemba, 2025 jijini Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (wa kwanza kushoto) akiteta jambo
na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi (wa pili kushoto) wakati wa ziara ya
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Ridhiwani Kikwete kwenye Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma tarehe 24. Novemba,
2025 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma katika ziara yake ya kikazi leo Tarehe 24, Novemba, 2025
1Menejimenti ya Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao katika ziara yake ya kikazi katika Ofisi hiyo leo jijini Dodoma.
1 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray wakiwa wanamsubiri Waziri wa Ofisi hyo Mhe. Ridhiwani Kikwete kuwasili katika Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma ambapo alikuwa na ziara ya kikazi leo tarehe 24 November,2025 kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Regina Qwaray akisaini kitabu cha wageni baada ya
kuwasili katika Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma katika ziara yake ya kikazi
leo Tarehe 24, Novemba, 2025
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Menejimenti ya
watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma (hawapo pichani) wakati wa ziara yake
ya kikazi katika Ofisi hiyo leo tarehe 24 Novemba, 2025
jijini Dodoma.









No comments:
Post a Comment