Na. Veronica Mwafisi-Manispaa ya Tabora
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka Viongozi
mkoani Tabora kuzingatia vigezo vya kuwapata walengwa wa Mpango wa Kunusuru
Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Mhe. Kikwete amesema moja ya jambo kubwa
ambalo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akilisisitiza ni kusaidia
Watanzania walio wanyonge. “TASAF awamu zilizopita illishia mwaka jana mwezi wa
9 lakini kwa upendo wake amepambana kuhakikisha fedha zinapatikana ili kusaidia
Watanzania hao kuepukana na umaskini,” Mhe. Kikwete ameongeza.
Akizungumza na Wananchi katika Manispaa ya
Tabora tarehe 9 Julai, 2026, baada ya kuhitimisha ziara yake kwa siku ya leo
aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya
Tabora na Manispaa ya Tabora ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo,
Mhe. Ridhiwani amesema sio sawa fedha hizo zikatumika kinyume kwa kuwaingiza
kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini watu wasiostahili. “Niwaombe mliopewa
dhamana ya kusimamia zoezi hili kutenda haki kwa kuwaweka walengwa stahiki,”
Mhe. Kikwete ameongeza.
Amesema kuna baadhi ya maeneo yalilalamikiwa
kwa kufanya mambo ya ajabu na kutowatendea haki walengwa katika fedha
walizokuwa wakipewa, niwaombe sana, tunapoanza mpango unaokuja, nisingependa
yale mapungufu yaliyojitokeza kipindi cha nyuma yajirudie.
Ametoa wito kwa Wananchi kushiriki katika
mikutano ya kutambua walengwa ili wapatikane watu sahihi. “Wananchi nanyi kwa
kuwa mnashiriki katika mikutano ya kuibua walengwa, mkisomewa majina ya
walengwa kama kuna ambao wameachwa mseme ili waongezwe na kama wamewekwa
wasiostahili pia mseme ili watolewe kwani mkikaa kimya ndio matokeo yake
wanaingizwa wasiostahili na baadae kuleta malalamiko.” ameongeza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Wananchi kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Sehemu ya Wananchi katika Manispaa ya Tabora wakimsikiliza Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa
ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya
Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa ya Tabora iliyolenga
kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akifurahia
jambo na Mjasiriamali wakati Waziri huyo
alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa
ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Wazee wa Manispaa ya Tabora wakati Waziri huyo
alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri
huyo aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya
ya Tabora na Manispaa ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya
maendeleo.
Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na Wananchi wa Manispaa ya Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa
ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Sehemu ya Wananchi katika Manispaa ya Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akicheza nyimbo ya ukaribisho katika
Manispaa ya Tabora alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa
ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.







No comments:
Post a Comment