Na. Rainer Budodi-Arusha
Tarehe 13 Oktoba, 2023
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi
na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman amesema kuwa uongozi ni kujitambua na ni dhamana, hivyo busara na hekima
inatakiwa zaidi katika kufanya uamuzi ili kutoathiri utendaji kazi.
Waziri Haroun amesema hayo leo tarehe 13 Oktoba, 2023
wakati akifunga Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika katika Ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano Jijini Arusha (AICC).
Mhe. Haroun amewasisitiza Wakuu wa Idara za Utawala na
Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kuepuka kutumia nguvu
katika usimamizi wa watumishi kwa kuwa hekima, busara, diplomasia na demokrasia
zina matokeo chanya wakati wote wa kuongoza watu.
“Si kwamba sisi ni bora zaidi kuliko watumishi wengine
lakini tumeaminiwa na Serikali na kupewa dhamana ya kusimamia watumishi wengine
katika taasisi zetu. Hivyo, nawaomba kila mmoja atambue kuwa binadamu yeyote
anataka kutambuliwa na kuheshimiwa wakati wote anapokuwa akitekeleza majukumu
ya taasisi na Serikali kwa jumla” aliongeza.
Amesema ni imani yake kuwa katika kikao kazi hicho,
washiriki wamepata nafasi ya kubadilishana uzoefu na kuelimishana kuhusu
taratibu zinazopaswa kufuatwa katika kushughulikia masuala mbalimbali ya
utawala na usimamizi wa rasilimaliwatu katika utumishi wa umma, hivyo watakaporudi
katika vituo vyao vya kazi watatumia uzoefu huo kutekeleza majukumu yao kwa
mujibu wa taratibu.
Naye, Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi
amesema kikao hicho kimejadili changamoto zinajitokeza katika utekelezaji wa
majukumu ya utawala na usimamizi wa rasilimaliwatu na namna bora ya kukabiliana
nazo kwa pamoja.
Kikao kazi hicho cha siku tatu kimehitimishwa leo kwa kuweka maazimio mbalimbali ya kuboresha usimamizi wa rasilimaliwatu na utawala katika utumishi wa umma.
Sehemu ya Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika
Utumishi wa Umma na watendaji wengine wa Serikali wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora SMZ, Mhe. Haroun Ali
Suleiman alipokuwa akizungumza nao wakati akifunga kikao kazi cha wakuu hao leo
tarehe 13/10/2023 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw.
Xavier Daudi akiwasilisha taarifa ya namna kikao kazi cha siku tatu cha Wakuu
wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma
kilivyofanyika kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi
na Utawala Bora SMZ, Mhe. Haroun Ali Suleiman kufunga kikao kazi cha leo tarehe
13/10/2023 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongella akitoa salamu za mkoa wake kabla
ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na
Utawala Bora SMZ, Mhe. Haroun Ali Suleiman kufunga kikao kazi cha Wakuu wa
Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma leo
tarehe 13/10/2023 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI pamoja na Wakuu
wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora SMZ,
Mhe. Haroun Ali Suleiman alipokuwa akihitimisha kikao kazi cha wakuu hao leo
tarehe 13/10/2023 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora
SMZ, Mhe. Haroun Ali Suleiman akisisitiza jambo kwa Wakuu wa Idara za Utawala
na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakati akifunga kikao
kazi cha wakuu hao leo tarehe 13/10/2023 katika Kituo cha Kimataifa cha
Mikutano Arusha (AICC).
Sehemu ya Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika
Utumishi wa Umma na watendaji wengine wa Serikali wakimsikiliza Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora SMZ, Mhe. Haroun Ali
Suleiman alipokuwa akizungumza nao wakati akifunga kikao kazi cha wakuu hao leo
tarehe 13/10/2023 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).
No comments:
Post a Comment