Monday, October 16, 2023

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAMPONGEZA MTUMISHI WAKE KWA KUIBUKA KIDEDEA KATIKA MBIO ZA BAISKELI

  • Na. Lusungu Helela-Dodoma
  • 16 Oktoba, 2023 

 

Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imempongeza mtumishi wa ofisi hiyo, Bw. Omari Ligoneko kwa  kuibuka  mshindi wa kwanza  kwenye mchezo wa mbio za baiskeli kwenye  mashindano ya Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yaliyomalizika hivi karibuni Mkoani Iringa.

 

Aidha katika mashindano hayo, Ofisi hiyo  iliibuka mshindi wa nne kwenye mbio za mita 100 na mshindi wa tano  mbio za mita 200.

 

Akitoa pongezi hizo, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, UTUMISHI, ACP Ibrahim Mahumi amesema Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora inajivunia kwa ushindi huo ambao ni heshima kubwa kwao. 

 

"Mimi pamoja na Wajumbe wa Menejimenti tumeona ni vema tukakuita ili tukae pamoja na kukupongeza kwani tumetambua mchango wako ambao umeiletea heshima Ofisi,” Bw. Mahumi amesema.

 

Awali, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais, UTUMISHI, Bw. Musa Magufuli amempongeza Bw.Ligoneko na kuahidi kuwa ofisi yake itaendelea kujiimarisha zaidi katika michezo ili kipindi kijacho iweze kutwaa vikombe vingi zaidi.

 

“Mwaka huu licha ya kubeba kikombe kimoja lakini tumejitahidi sana ukilinganisha na miaka mingine, tumejipanga tutaanza mazoezi mapema ili mwakani tunyakue vikombe vingi zaidi,” Bw. Magufuli ameongeza.

 

Kwa upande wake, Mshindi huyo, Bw. Omari Ligoneko ameishukuru Menejimemti kwa kumpa heshima hiyo ya kuwa pamoja naye licha ya majukumu mengi yanayowakabili.

 

‘’Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Uongozi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa kutupatia kibali cha kushiriki michezo ya SHIMIWI na Timu nzima ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa ushirikiano waliouonyesha  wakati wote wa michezo na hatimaye kuweza kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio za baiskeli,” Bw. Ligoneko amesema.

 



Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, ACP Ibrahim Mahumi akizungumza na wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi hiyo mara baada ya Bw. Omari Ligoneko kukabidhi kombe kufuatia kuibuka mshindi wa kwanza katika mchezo wa mbio za baiskeli kwenye mashindano ya 37 ya Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yaliyomalizika hivi karibuni mkoani Iringa.

 

Mshindi wa kwanza katika mchezo wa mbio za baiskeli kwenye mashindano ya 37 ya Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Bw. Omari Ligoneko akizungumza mbele ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora

 

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais- UTUMISHI, Bw. Musa Magufuli akizungumza na wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi hiyo mara baada ya Bw.Omari Ligoneko kukabidhi kombe la ushindi wa kwanza katika mchezo wa mbio za baiskeli kwenye mashindano ya 37 ya Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yaliyomalizika hivi karibuni mkoani Iringa.

 

Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti wakifurahi wakati Mshindi wa kwanza katika mchezo wa mbio za baiskeli kwenye mashindano ya 37 ya Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Bw. Omari Ligoneko alipokuwa akiweka kombe katika meza mbele ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi hiyo.

Mshindi wa kwanza katika mchezo wa mbio za baiskeli kwenye mashindano ya 37 ya Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Bw. Omari Ligoneko akiwa ameshika kombe mara baada ya tukio la kukabidhi mbele ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI.

 

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, ACP Ibrahim Mahumi akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli, Bw. Omari Ligoneko mara baada ya tukio la kukabidhi kombe kwa wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, UTUMISHI, ACP Ibrahim Mahumi akiwa ameshika kombe akiwa na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi hiyo mara baada ya tukio la kukabidhi kikombe hicho kwa Wajumbe hao

 

 

Mkurugenzi, Idara ya Uendelezaji Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda akiwa ameshika kombe akiwa na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi hiyo mara baada ya tukio la kukabidhi kombe hilo kwa Wajumbe hao.

 


 
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais- UTUMISHI, Bw. Musa Magufuli akiwa ameshika kombe akiwa na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi hiyo mara baada ya tukio la kukabidhi kombe hilo kwa Wajumbe hao.

 

 

No comments:

Post a Comment