Monday, January 14, 2019

BODI YA MISHAHARA YATAKIWA KUTOFANYA KAZI KIMAZOEA KATIKA KUTEKELEZA JUKUMU LAKE LA MSINGI LA KUISHAURI SERIKALI NAMNA BORA YA KUOANISHA NA KUWIANISHA MISHAHARA NA MASILAHI YA WATUMISHI WA UMMA NCHINI



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi na wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi alipowatembelea  ofisini kwao makao makuu ya bodi jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Mariam G. Mwanilwa, akieleza  majukumu ya Bodi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi na Naibu Waziri huyo na watumishi  na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi  katika  Utumishi wa Umma cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bw. Donald S.B. Ndagula akifafanua majukumu ya bodi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi na Naibu Waziri huyo na watumishi  na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi  katika  Utumishi wa Umma cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi na Naibu Waziri huyo na watumishi na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Masilahi  katika  Utumishi wa Umma cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe na watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma mara baada ya kumalizika kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi na Wajumbe wa Bodi hiyo ya Mishahara na Masilahi  katika  Utumishi wa Umma cha kuhimiza uwajibikaji  kilichofanyika Makao Makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment