Thursday, June 8, 2023

MHE. SIMBACHAWENE AFANYA KIKAO KAZI NA MAKAMISHNA WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA KUHIMIZA UWAJIBIKAJI



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na Makamishna hao kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.

Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (aliyesimama) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Makamishna hao kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.


Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe. Jaji (Mst.) Hamisa Kalombola akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene kabla ya Waziri huyo kuzungumza na Makamishna wa Tume hiyo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kushoto) akimsikiliza mmoja wa Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma (hayupo pichani) wakati akitoa neno la shukrani kwa Waziri huyo kwenye kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Makamishna hao. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe. Jaji (Mst.) Hamisa Kalombola.


Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe. Balozi John Haule akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene mara baada ya Waziri huyo kuzungumza nao kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma mara baada ya kuhitimisha kikao kazi chake na Makamishna hao kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji. Wa pili kushoto waliokaa ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe. Jaji (Mst.) Hamisa Kalombola na wa pili kulia waliokaa ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Mathew Kirama.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akikaribishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Mhe. Jaji (Mst.) Hamisa Kalombola kushiriki kikao kazi kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.



No comments:

Post a Comment