Tuesday, July 12, 2016

MATUKIO: ZIARA YA MHE. KAIRUKI MKOANI TANGA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akifuatilia taarifa ya mkoa wa Tanga iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu Tawala Msaidizi, Utawala Na Rasilimaliwatu, Bwana Bernard Marcelline wakati wa kikao kazi na Viongozi wa mkoa wa Tanga kilichofanyika tarehe 11/7/2016 ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Tanga. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigela na kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Injinia Zena Said.
Baadhi ya Watumishi wa Mkoa wa Tanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika tarehe 11/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiongea na Waandishi wa Habari baada ya kikao kazi na watumishi wa mkoa wa Tanga kilichofanyika tarehe 11/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Bwana Issa Ng’imba akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yalioulizwa na watumishi wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na watumishi wa mkoa wa Tanga kilichofanyika tarehe 11/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Henry Mambo, akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yalioulizwa na watumishi wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na watumishi wa mkoa wa Tanga kilichofanyika tarehe 11/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga.


No comments:

Post a Comment