Baadhi ya Watumishi
wa Mkoa wa Morogoro wakiwa katika kikao kazi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) kilichofanyika
tarehe 15/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Mkoa wa Morogoro
Waziri waNchi, Ofisi yaRais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. AngellahKairuki (Mb)
amewataka Watendaji wa Taasisi za Serikali kusimamia suala zima la watumishi na
wadau kupata mrejesho wa barua wanazozituma kwenye taasisi zao.
Mhe. Kairuki ameyasema hayo leo
wakati wa kikao kazi na watumishi wa mkoa wa Morogoro kilichofanyika katika ukumbi
wa Manispaa ya Mkoa wa Morogoro.
Mhe. Kairuki amesema kumekuwa
na malalamiko mengi sana ya watumishi na wadau kutopata mrejesho wa barua wanazozituma
kwenye taasisi za Serikali na hata wakijibiwa sio kwa wakati.
“Tunataka barua zijibiwe mara
tu mzipatapo, hata kukiri kupokea pia ni mrejesho hivyo ni vema tukajibu barua na
kwa wakati”Mhe. Kairuki alisisitiza.
Aidha, Mhe. Kairuki amewaagiza
Watendaji hao kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara kwenye masija la za ofisi zao
ili kuboresha utoaji huduma kwa umma.
Amesema eneo la ofisi za Masijala
limekuwa likilalamikiwa kwa kiasi kikubwa kwa majalada kutoonekana na kusababisha
watumishi na wadau kutopata mrejesho.
“Tutoe mwongozo kwa watumishi
wa Masijala na tusiwaache bila kuwafuatilia kwani eneo hili limekuwa likilalamikiwa
sana. Ikiwezekana tufanye kaguzi za kushtukiza ili kuleta ufanisi katika kazi”
Mhe. Kairuki aliongeza.
Ameongeza kuwa ufuatiliaji
pia ufanyike kwa kila Ofisa ambaye anakaa na jalada kwa muda mrefu bila kutoa mrejesho.
Mhe. Kairuki amekutana na watumishi
wa Mkoa wa Morogoro ikiwa ni mwendelezo wa ziara alizozipanga kuzitekeleza mikoani
kwal engo la kusikiliza kero za watumishi ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi na kuangalia
ni namna gani ya kuweza kuboresha utendaji kazi Serikalini.
|
No comments:
Post a Comment