Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma.
Tarehe 08 Februari, 2021
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro, amewataka Watumishi wa Umma nchini kulinda afya
zao ili waweze kuwahudumia vema wananchi wanaofuata huduma mbalimbali katika
taasisi zao.
Dkt. Ndumbaro ametoa wito huo mapema leo wakati
akizungumza na Watumishi wa ofisi yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa
kukutana na watumishi hao kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Dkt. Ndumbaro amesema, ili Watumishi wa Umma waweze
kutekeleza majukumu yao kikamilifu, hawana budi kulinda afya zao ikizingatiwa
kuwa wakati wa utoaji huduma wanakutana
na watu ambao baadhi yao wanaweza kuwa na changamoto mbalimbali za kiafya.
Ili kuhakikisha taifa linakuwa na rasilimaliwatu yenye
tija, Dkt. Ndumbaro amewataka Watumishi wa Umma kuwa na utaratibu wa kupima
afya mara kwa mara na kupata tiba mapema iwezekanavyo pindi wanapohisi
kukabiliwa na changamoto yoyote ya kiafya.
Sanjali na hilo, Dkt. Ndumbaro amewahimiza Watumishi wa
Umma kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya kwa lengo la kuendelea
kutoa mchango katika ujenzi wa taifa.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma Dkt. Laurean Ndumbaro amekuwa na utaratibu wa kukutana na Watumishi wa
Umma katika maeneo mbalimbali nchini kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto
mbalimbali zinazowakabili.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Watumishi wa ofisi yake leo jijini
Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi hao kwa lengo
la kuhimiza uwajibikaji.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akisisitiza jambo kwa Watumishi wa ofisi yake leo
jijini Dodoma alipokutana nao kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Baadhi ya Watumishi wa Umma wa Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati
akizungumza nao leo jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
No comments:
Post a Comment