James K. Mwanamyoto-Mpwapwa
Tarehe 17 Februari, 2021
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amemtaka kila
Mtumishi wa Umma nchini kuwa na mpango kazi utakaomuwezesha kufanya kazi kwa
ufanisi na kutoa huduma bora kwa umma.
Mhe. Ndejembi ametoa maelekezo
hayo wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Mpwapwa na Kongwa mkoani Dodoma.
Mhe. Ndejembi amesema, ni jukumu
la Waajiri kuhakikisha kila mtumishi anatekeleza mpango kazi wake ili kutoa
mchango wa kiutendaji mahala pa kazi badala ya kuendelea kufanya kazi kwa
mazoea jambo ambalo halina tija katika maendeleo ya taifa.
Sanjali na hayo, Mhe. Ndejembi
amewasisitiza Watumishi wa Umma kuzingatia ujazaji wa fomu za Mfumo wa Wazi wa
Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) ili kutoa fursa kwa Waajiri kupima
utendaji kazi wa watumishi wao kwa lengo la kuwapa stahiki kulingana na utendaji
kazi wao.
“OPRAS ipo kwa mujibu wa Sera ya
Menejimenti na Ajira ya Mwaka 1998 kama ilivyorekebishwa Mwaka 2008 pamoja na
Sheria ya Utumishi Sura Namba 298, hivyo ni jukumu la waajiri kuhakikisha
watumishi wanajaza fomu na kufanyiwa tathmini ya utendaji kazi wao ili kuongeza
ufanisi kiutendaji.” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Akijibu hoja ya Bw. Kandindo Mumeli,
mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuhusu baadhi ya waajiri kutotenga
bajeti ya kuwahudumia Watumishi wa Umma wenye Ulemavu kama Mwongozo wa Huduma
kwa Watumishi wa Umma wenye Ulemavu wa Mwaka 2008 unavyoelekeza, Mhe. Ndejembi
amewataka Waajiri kutoa kipaumbele cha kutenga fedha za kuwahudumia watumishi
hao ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Aidha, Mhe. Ndejembi amesisitiza
juu ya usimamizi wa ruzuku inayotolewa na Serikali kwa wanufaika wa Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini, ambapo amesema, ni jukumu la kila Mtumishi wa Umma kuhakikisha
fedha wanazopokea wanufaika wa TASAF zinatumika kuboresha maisha yao kwa
kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo.
“Kumekuwa na mtazamo hasi juu ya
usimamizi wa fedha za TASAF kuwa ni jukumu la Waratibu wa TASAF pekee, jambo
ambalo halina tija kwa taifa kwani usimamizi wa fedha za umma ni jukumu la kila
mtumishi, hivyo ni wajibu wetu sote kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa
malengo yaliyokusudiwa.” Mhe. Ndejembi ameongeza.
Pia, Mhe. Ndejembi amepiga
marufuku kitendo cha kukata fedha za wanufaika wa TASAF ili kuchangia Mfuko wa
Afya ya Jamii (CHF) kwani kitendo hicho kinawakwamisha wanufaika kutumia ruzuku
waliyopewa katika shughuli mbalimbali za maendeleo zitakazoboresha maisha yao.
Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa,
wanufaika wa TASAF waachwe huru kutumia ruzuku wanazopatiwa katika shughuli
mbalimbaliz za maendeleo ili watakachozalisha ndio wakitumie kuchangia CHF kwa
hiari.
Lengo la
ziara ya Mhe. Ndejembi katika Wilaya hizo ilikuwa ni kutatua changamoto
zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na usimamizi mzuri wa
utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na
Watumishi Wilayani Mpwapwa wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutatua
changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na
usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mpwapwa wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipokuwa
akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la
kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na
usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.
Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Mpwapwa, Bw. Kandido Mumeli Akiwasilisha hoja ya kiutumishi kwa Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la
kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na
usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akijibu
hoja ya Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Kandido Mumeli
aliyoiwasilisha wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la
kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na kuhimiza uwajibikaji na
usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi
akizungumza na Watumishi Wilayani Kongwa wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la

No comments:
Post a Comment