Tuesday, February 23, 2021

NDEJEMBI AHIMIZA WAKALA YA NDEGE ZA SERIKALI KUBORESHA UTOAJI HUDUMA

James K. Mwanamyoto-Dar es Salaam

Tarehe 23 Februari, 2021

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewahiza Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuboresha huduma zitolewazo na Wakala hiyo.

Mhe. Ndejembi ametoa wito huo leo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wakala hiyo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kujitambulisha, kufahamu kwa kina makujumu ya Wakala hiyo, kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili watumishi wa Wakala hiyo na kuhimiza uwajibikaji.

Mhe. Ndejembi amewapongeza Watumishi wa Wakala hiyo kwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na weledi kwani hakuna maafa yoyote yaliyowahi kujitokeza tangu Serikali ianze kumiliki ndege zake. 

Mhe. Ndejembi amesema, Wakala hiyo ina jukumu kubwa la kuhakikisha matengenezo ya ndege yanafanyika kwa wakati ili ziendelee kutoa huduma ya usafiri wa anga kwa Mhe. Rais na Viongozi Wakuu wa Serikali kwa lengo la kuhakikisha shughuli za Viongozi hao wa Kitaifa zinatekelezwa kama zilivyopangwa.

Aidha, Mhe. Ndejembi ameahidi kuzifanyia kazi changamoto za Wakala hiyo ili kuwawezesha Watumishi wa Wakala hiyo kuwa na mazingira bora yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Mhe. Ndejembi amewaasa watumishi hao kuendelea kuchapa kazi wakati changamoto zao zikifanyiwa kazi.

Wakala ya Ndege za Serikali ilianzishwa tarehe 17 Mei, 2002 kwa mujibu wa Sheria ya Wakala ya Ndege za Serikali Na.3 ya Mwaka 1997 kwa lengo la kuboresha huduma na kuimarisha usalama wa usafiri wa ndege kwa Viongozi Wakuu wa Kitaifa wanaotumia ndege hizo. Pamoja na jukumu hilo, Wakala ina jukumu la kuratibu kwa niaba ya Serikali ununuzi wa ndege mpya za biashara, kuzikodisha kwa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) na kusimamia mikataba ya ukodishwaji wa ndege hizo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Watumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.



Mtumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA), Salahe Harun Mwanauta ambaye ni Rubani akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.


Mtumishi wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA), Bernard Joseph Mayila akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Menejimenti ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.


Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) Dkt. Benjamin Ndimila akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wakala yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala hiyo leo Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.



No comments:

Post a Comment