Saturday, December 29, 2018

UTUMISHI YAUNGA MKONO KWA VITENDO KAMPENI YA MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA SULUHU YA KULIFANYA JIJI LA DODOMA KUWA KIJANI KWA KUPANDA MITI



Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza kuhusu ofisi yake kuunga mkono kwa vitendo kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa la kijani  iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan  mara baada ya watumishi wa ofisi yake (hawapo pichani) kukamilisha zoezi la upandaji miti katika ofisi inayojengwa Ihumwa kwenye mji wa serikali jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mathew Kirama akishiriki katika zoezi la upandaji miti Ihumwa katika mji wa serikali jijini Dodoma, eneo ambalo Ofisi ya Rais-Utumishi inajengwa ili kutoa huduma kwa umma.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph akishiriki kuchimba mashimo kwa ajili  kupanda miti Ihumwa katika mji wa serikali jijini Dodoma, eneo ambalo Ofisi ya Rais-Utumishi inajengwa ili kutoa huduma kwa umma.

Baadhi ya  watumishi wa  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakiwa tayari  kupanda miti katika ofisi inayojengwa Ihumwa kwenye mji wa serikali jijini Dodoma ili kuunga mkono kwa vitendo kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa la kijani,  iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan Julai 21,2017.

No comments:

Post a Comment