Thursday, December 20, 2018

DKT. MWANJELWA AKUTANA NA WATUMISHI WA IDARA YA UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALIWATU NA KUHIMIZA UWAJIBIKAJI

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa   Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (hawapo pichani) alipoitembelea idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

Kaimu Mkurugenzi,  Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Musa Joseph(aliyesimama) akifafanua majukumu ya idara yake kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kushoto) alipoitembelea idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora alipoitembelea idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

No comments:

Post a Comment