Na. James K.
Mwanamyoto-Dar es Salaam
Tarehe 10 Mei,
2022
Tanzania imependekezwa na Sekretarieti ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika kufanyiwa majaribio ya matumizi ya Nyenzo ya Tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa Afrika wa Maadili na Misingi ya Utumishi wa Umma na Utawala ambayo itakuwa ikitumika kuzitathmini nchi wanachama za Umoja wa Afrika.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo wataalam kutoka Tanzania Bara
na Zanzibar ya namna bora ya kutumia Nyenzo hiyo ya Tathmini ya
utekelezaji wa Mkataba wa Afrika wa Maadili na Misingi ya Utumishi wa Umma na
Utawala.
Mhe. Jenista amesema Umoja wa
Afrika (AU) umeliheshimisha taifa letu kwa kutoa fursa ya kuwa nchi ya kwanza
Barani Afrika kufanyiwa majaribio ya kutumia Nyenzo ya Tathmini ya utekelezaji
wa Mkataba wa Afrika wa Maadili na Misingi ya Utumishi wa Umma na Utawala, ambao utaziwezesha Nchi Wanachama kuandaa taarifa
itakayokuwa ikizingatia misingi iliyoainishwa kwenye Mkataba huo.
Waziri Jenista amesema, Nchi
Wanachama za Umoja wa Afrika zilikubaliana kutengeneza Nyenzo ambayo itatumika
kusaidia kupima utekelezaji wa Mkataba wa Afrika wa Maadili na Misingi ya
Utumishi wa Umma na Utawala katika nchi zote wanachama.
Mhe. Jenista ameongeza kuwa,
Mkataba huo unahimiza uzingatiaji wa maadili katika Utumishi wa Umma katika
maeneo mbalimbali likwemo eneo la mapambano dhidi ya rushwa, uzingatiaji wa sheria
na utawala bora kwa ujumla.
Waziri Jenista amesema, semina
hiyo ni fursa ya kipekee kwa Watendaji wa pande zote mbili za Muungano kwenye
Ofisi zinazoshughulikia masuala ya Utumishi wa Umma kuangalia ni kwa namna gani
wataweza kuitumia Nyenzo hiyo vizuri katika kuandaa ripoti ambayo itawasilishwa
Umoja wa Afrika.
“Jambo kubwa hapa, ni nchi
yetu kuwa ya kwanza kuitumia Nyenzo hiyo, kupata mafunzo ya kuitumia pamoja na
kuwa wa kwanza kutathminiwa kwa namna
gani tumeitumia Nyenzo hiyo kuandaa taarifa itakayowasilishwa Umoja wa Afrika.”
Mhe. Jenista ameongeza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara
ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora ambaye Idara yake ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa Mkataba huo, Bi.
Agnes Meena amesema baada ya kukamilika kwa semina hiyo, wanatarajia kuandaa
taarifa nzuri ya nchi itakayokuwa ya kwanza Afrika kwa kutumia Nyenzo ya
Tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa Afrika wa Maadili na Misingi ya Utumishi
wa Umma na Utawala.
Naye Mshiriki wa semina hiyo
kutoka Tanzania Bara, Bw. Romwald Rwamarumba amesema Tanzania imekuwa ni nchi
ya kwanza Barani Afrika kufanyiwa majaribio ya kutumia Nyenzo hiyo, hivyo
taarifa itakayoandaliwa na nchi itakuwa ya kwanza Barani Afrika ilizozingatia
misingi iliyowekwa kwa mujibu wa Mkataba.
Ameongeza kuwa, taarifa hiyo
itatumiwa pia na nchi wanachama Barani Afrika kama rejea ya uandaaji wa taarifa
za utekelezaji wa mkataba huo kwenye nchi zao.
Kwa upande wake mshiriki
kutoka Zanzibar, Bi. Fatma Saadalla amesema, semina hiyo itasaidia kuwajengea
uelewa wa Mkataba huo na namna ya kutumia Nyenzo iliyopendekezwa kufanya
tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa Afrika wa Maadili na Misingi ya Utumishi
wa Umma na Utawala.
Semina hiyo ya siku nne
imeandaliwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
kwa kushirikiana na Kamisheni ya Umoja wa Afrika na imewashirikisha wajumbe
kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifungua
semina ya kuwajengea uwezo wataalam kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wa namna
bora ya kutumia Nyenzo ya Tathmini ya utekelezaji wa Mkataba
wa Afrika wa Maadili na Misingi ya Utumishi wa Umma na Utawala iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
Wataalam kutoka
Tanzania Bara na Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo wataalam hao juu ya namna
bora ya kutumia Nyenzo ya Tathmini ya utekelezaji wa Mkataba
wa Afrika wa Maadili na Misingi ya Utumishi wa Umma na Utawala iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa
Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bw. Issaka Garba Abdou akielezea sababu ya Tanzania
kupendekezwa na Sekretarieti ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika kufanyiwa
majaribio ya matumizi ya Nyenzo ya Tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa Afrika
wa Maadili na Misingi ya Utumishi wa Umma na Utawala wakati wa semina ya
kuwajengea uwezo wataalam kutoka Tanzania Bara na Zanzibar iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa
Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala bora, Bi. Agnes Meena akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kufungua semina ya kuwajengea uwezo wataalam kutoka Tanzania
Bara na Zanzibar juu ya namna bora ya kutumia Nyenzo ya Tathmini ya
utekelezaji wa Mkataba wa Afrika wa Maadili na Misingi ya Utumishi wa Umma na
Utawala iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na
wataalam kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wanaoshiriki semina ya
kujengewa uwezo wa kutumia Nyenzo ya Tathmini ya utekelezaji wa
Mkataba wa Afrika wa Maadili na Misingi ya Utumishi wa Umma na Utawala iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mipango Rasilimaliwatu kutoka Ofisi ya Rais-Katiba
Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Fatma Mzee Saadalla akielezea
umuhimu wa semina ya kuwajengea uwezo wa kutumia
Nyenzo ya Tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa Afrika wa Maadili na Misingi ya
Utumishi wa Umma na Utawala iliyoanza leo jijini
Dar es Salaam.
Afisa Utumishi kutoka Ofisi ya Rais-Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Tanzania Bara, Bw. Romwald Rwamarumba, Tanzania
Bara, Bw. Romwald Mwamarumba akielezea umuhimu wa semina ya kuwajengea uwezo wa kutumia Nyenzo ya Tathmini ya
utekelezaji wa Mkataba wa Afrika wa Maadili na Misingi ya Utumishi wa Umma na
Utawala iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment