Na Eric Amani, Dodoma
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma
Mkomi ameongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Ufuatiliaji na Tathmini kilichojadili
Taaifa ya Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Rais – Utumishi
kwa Robo ya Nne ya Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Kikao
hicho kimefanyika leo Septemba 01, 2026 katika ukumbi wa Nyaraka Jijini Dodoma
kwa lengo la kupitia na kutathmini kiwango cha utekelezaji wa majukumu,
mipango, shughuli na malengo yaliyowekwa na Ofisi katika kipindi cha robo ya
nne ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Akizungumza
wakati wa kikao hicho, Bw. Mkomi amesisitiza umuhimu wa ufuatiliaji na tathmini
katika kuhakikisha kuwa mipango na shughuli za Ofisi zinatekelezwa kwa ufanisi,
kwa wakati na kwa kuzingatia viashiria vya utendaji vilivyowekwa.
Amesema
ufuatiliaji na tathmini ni nyenzo muhimu katika kupima matokeo ya utekelezaji
wa mipango ya Serikali, kutambua maeneo yanayohitaji maboresho na kuwezesha
uongozi kufanya maamuzi yanayozingatia ushahidi.
“Ni
muhimu taarifa za ufuatiliaji na tathmini zisitumike tu kwa ajili ya kuonesha
kiwango cha utekelezaji, bali pia ziwe msingi wa kufanya maboresho na kuchukua
hatua stahiki pale ambapo utekelezaji haujafikia malengo yaliyokusudiwa,”
amesema Bw. Mkomi.
Katika
hatua nyingine, amewataka viongozi na watendaji wa Ofisi kuhakikisha
utekelezaji wa majukumu yao unaendana na mipango na vipaumbele vilivyowekwa,
huku wakizingatia matumizi bora ya rasilimali, uwajibikaji na utoaji wa huduma
zenye tija kwa wananchi.
Pamoja na mambo mengine, kamati pia imejadili maeneo yanayohitaji kuimarishwa katika kipindi kijacho, ikiwemo kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa mipango, kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli na kuhakikisha taarifa za utendaji zinawasilishwa kwa wakati na kwa kuzingatia viashiria vilivyowekwa.
![]() |
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais – UTUMISHI Bw. Juma Mkomi akizungumza na viongozi mbalimbali
wa Ofisi ya Rais – UTUMISHI wakati wa Kikao cha Kamati Kuu ya Ufuatiliaji na
Tathmini katika Ukumbi wa Nyaraka Jijini Dodoma Agosti 1, 2026 |
![]() |
Baadhi
ya Wakurugenzi kutokea Ofisi ya Rais – UTUMISHI wakifatilia Kikao cha Kamati
Kuu ya Ufuatiliaji na Tathmini katika Ukumbi wa Nyaraka Jijini Dodoma Agosti 1,
2026 |
![]() |
Meneja
Mipango na Maendeleo Bi. Mwanaidi Mdee kutokea Chuo Cha Utumishi wa Umma (TPSC)
akiwasilisha mada katika Kikao cha Kamati Kuu ya Ufuatiliaji na Tathmini
Septemba 1, 2026 |






No comments:
Post a Comment