Monday, September 21, 2026

KATIBU MKUU MKOMI ATOA WITO WA KUPIMA AFYA ILI KUONGEZA TIJA, UFANISI NA UWAJIBIKAJI MAHALI PA KAZI

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 21 Septemba, 2026.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi ametoa wito kwa Watumishi wa Umma kupima afya zao mara kwa mara ili kujijua na kuona namna bora ya kuishi kwa lengo la kuongeza tija, ufanisi na uwajibikaji mahali pa kazi kwa maslahi mapana ya nchi.

Bw. Mkomi ametoa wito huo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo katika eneo maalum la mafunzo mara baada ya madaktari kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), kutoa mafunzo kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi.

“Kupima afya mara kwa mara kunasaidia kujikinga na mambo mengi ikiwemo kubadilisha mtindo wa maisha, hivyo ni muhimu Watumishi wa Umma tukajenga utamaduni wa kuangalia afya zetu bila kulazimishwa,” amesisitiza Katibu Mkuu Mkomi.

Aidha, Katibu Mkuu Mkomi amewahimiza watumishi hao kwenda kwa wakati katika maeneo maalum ya ofisi hiyo yaliyotengwa kwa ajili ya kupima afya na kutoa ushirikiano kwa wataalam wa Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) waliofika kutoa huduma hiyo.  

Awali, Daktari kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), Bw. Mkubwa Suleiman alisema ni muhimu watumishi hao wakazingatia mazoezi na mlo kamili utakaowafanya kuwa na afya bora ambayo ni nguzo muhimu kwa kila mtu.

Kwa upande wake, Daktari Adam Hussein pia kutoka katika Taasisi hiyo alisema, Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wana majukumu mengi ikiwemo utoaji wa huduma mbalimbali za kiutumishi hivyo, ni muhimu kila mtumishi akajua afya yake ili waweze kutoa huduma bora kwa Wananchi wakiwa na utimamu wa afya.

Wataalam hao wamelenga kutoa huduma mbalimbali kwa watumishi wa ofisi hiyo ikiwemo huduma ya mifupa, mgongo, mishipa ya fahamu, magonjwa ya ndani pamoja na mazoezi ya tiba na lishe.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo (hawapo pichani) alipokuwa akihitimisha mafunzo yaliyolenga kuwajengea Watumishi hao uelewa kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyotolewa na Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakisikiliza mada kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyotolewa na Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakisikiliza mada kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyotolewa na Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma. Waliopo mstari wa mbele ni Watumishi kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI).


Daktari kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), Bw. Adam Hussein akisisitiza jambo wakati wa mafunzo yaliyotolewa na taasisi hiyo kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyofanyika Ofisi ya Rais-UTUMISHI leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika eneo maalumu Mtumba, jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (wapili kutoka kushoto) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, wa ofisi hiyo, Bi. Nyasinde Mukono (wakwanza kushoto) wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyofanyika katika ofisi hiyo leo tarehe 21 Septemba, 2026 Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakisikiliza mada kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyotolewa na Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Nyasinde Mukono akizungumza jambo wakati akimkaribisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) kuzungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Daktari kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), Bw. Mkubwa Suleiman akisisitiza jambo wakati wa mafunzo yaliyotolewa na taasisi hiyo kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyofanyika Ofisi ya Rais-UTUMISHI leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika eneo maalumu Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakisikiliza mada kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyotolewa na Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia mada kuhusu umuhimu wa lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyotolewa na Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.

 



No comments:

Post a Comment