Friday, September 25, 2026

NAIBU KATIBU MKUU LWANGILI AIPONGEZA MOI KWA KUENDESHA KLINIKI YA UPIMAJI AFYA, AAHIDI KUONGEZEKA KWA ARI YA UTENDAJI KAZI

Na. Antonia Mbwambo na Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 25 Septemba, 2026.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili ameishukuru Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kuendesha zoezi la upimaji afya na huduma za matibabu kwa watumishi wa ofisi hiyo ambayo itasaidia uimara wa afya za watumishi hao na kuongeza ari ya utendaji kazi.

Bi. Lwangili ametoa rai hiyo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na Watumishi na Madaktari hao katika eneo maalum mara baada ya kuhitimisha rasmi zoezi la upimaji afya na matibabu kutoka kwa madaktari bingwa wa Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI).

“Niwahakikishie mbegu mliyoipanda mtaivuna, mtaona matokeo ya uimara zaidi wa afya za watumishi wetu, wiki nzima tumeona watumishi wengi wakishiriki katika zoezi la upimaji afya na kupatiwa matibabu, tunaishukuru sana Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) tunaamini afya za watumishi hawa zitakuwa imara zaidi na itaongeza ari ya utendaji kazi,” amesema Bi. Lwangili

Aidha, Bi. Lwangili amewapongeza watumishi wa ofisi hiyo kwa kuwatumikia watumishi wa umma wenzao na wananchi waliofika kupata huduma katika ofisi hiyo pamoja na kwamba walikuwa katika zoezi la upimaji wa afya lakini huduma nyingine za kiutumishi ziliendelea kutekelezwa kwa wakati.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Musa Magufuli amesema Ofisi ya Rais-UTUMISHI itaendelea kufanya mazoezi ya mara kwa mara hasa kwa siku mbili Jumanne na Alhamisi ambazo zimepangwa maalum kufanyika kwa mazoezi hayo baada ya muda wa kazi.

Bw. Magufuli ameahidi kuwa watumishi wa ofisi hiyo watakuwa mabalozi wazuri kwa watumishi wengine kwa lengo la kuimarisha afya zao.

Naye, Daktari Bingwa wa Upasuaji-Magonjwa ya Ubongo, Uti wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), Bw. Hamisi Shabani ameishukuru Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa ushirikiano mkubwa ambao wameuonyesha wakati taasisi hiyo ilipokuwa ikitoa huduma za upimaji wa afya na matibabu.

Ameongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa sana kwa watumishi hao kuzingatia mazoezi na kupata mlo kamili utakaowafanya kuwa na afya bora na kuwajengea utimamu katika utekelezaji wa majukumu yao kwa ustawi wa Taifa.

Kwa wiki nzima Wataalam kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) walitoa huduma mbalimbali kwa watumishi wa ofisi hiyo ikiwemo huduma ya mifupa, mgongo, mishipa ya fahamu, magonjwa ya ndani mazoezi ya tiba na lishe pamoja na ushauri nasaha.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili akizungumza na Watumishi na Madaktari mara baada ya kuhitimisha rasmi zoezi la upimaji afya, matibabu, lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyokuwa yakitolewa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (wapili kutoka kulia) akifanya mazoezi ya viungo pamoja na Watumishi mara baada ya kuhitimisha rasmi zoezi la upimaji afya, matibabu, lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyokuwa yakitolewa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Musa Magufuli.


Sehemu ya Viongozi na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (wapili kutoka kulia) kuhitimisha rasmi zoezi la upimaji afya, matibabu, lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyokuwa yakitolewa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Viongozi na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili kuhitimisha rasmi zoezi la upimaji afya, matibabu, lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyokuwa yakitolewa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bi. Prisca Lwangili (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati akihitimisha rasmi zoezi la upimaji afya, matibabu, lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyokuwa yakitolewa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Musa Magufuli (aliyevaa kofia kulia) akizungumza jambo na Daktari kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), Bw. Frank Mhonda (wakwanza kushoto) kabla ya kuanza kwa mazoezi ya viungo yaliyokuwa yakihitimisha zoezi la upimaji afya, matibabu, lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyotolewa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma. Wengine ni Watumishi wa Ofisi hiyo.


Sehemu ya Viongozi na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (hayupo pichani) kuhitimisha rasmi zoezi la upimaji afya, matibabu, lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyokuwa yakitolewa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.


Daktari kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), Bi. Dafrosa Kiria (kulia) akitoa elimu ya lishe bora kwa Mtumishi wa Ofisi hiyo wakati wa zoezi la upimaji afya, matibabu, lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyokuwa yakitolewa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.


Mtumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Lucy Kallaghe (kulia) akizungumza jambo na Mtoa huduma kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) wakati wa zoezi la upimaji afya, matibabu, lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyokuwa yakitolewa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (hayupo pichani) kuhitimisha rasmi zoezi la upimaji afya, matibabu, lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyokuwa yakitolewa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (hayupo pichani) kuhitimisha rasmi zoezi la upimaji afya, matibabu, lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyokuwa yakitolewa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.

Madaktari kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) wakiwaonyesha kwa vitendo Viongozi na Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora namna ya kufanya mazoezi kwa wanaokaa muda mrefu mara baada ya kukamilika kwa zoezi la upimaji afya, matibabu, lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyokuwa yakitolewa na madaktari hao yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.


Daktari Bingwa wa Upasuaji-Magonjwa ya Ubongo, Uti wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), Bw. Hamisi Shabani akionesha picha ya mazoezi yanayotakiwa kufanyika kwa wanaokaa muda mrefu mara baada ya kukamilika kwa zoezi la upimaji afya, matibabu, lishe bora na namna bora ya kufanya mazoezi yaliyokuwa yakitolewa na madaktari kutoka katika taasisi hiyo yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba, jijini Dodoma.

 









 

No comments:

Post a Comment