Monday, September 28, 2026

NAIBU KATIBU MKUU LWANGILI AWATAKA WATUMISHI KUZINGATIA UMUHIMU WA BIMA YA MAISHA

Na. Antonia Mbwambo – Dodoma

Tarehe 28 Septemba, 2026

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili, amewataka watumishi wa Ofisi hiyo kuzingatia umuhimu wa Bima ya Maisha katika kuweka akiba kwa ajili ya kutimiza malengo yao na wategemezi wao.

Bi. Lwangili ameyasema hayo Septemba 28, 2026 wakati akihitimisha mafunzo kuhusu Bima ya Maisha yaliyotolewa na wawezeshaji kutoka Shirika la Bima ya Taifa (NIC) kwa watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, yaliyolenga kuwaongezea uelewa, umuhimu, aina na faida za Bima ya Maisha.

Amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa watumishi kwani yanawaongezea uelewa kuhusu namna Bima ya Maisha inavyoweza kusaidia katika kukabiliana na changamoto za kifedha zinazoweza kujitokeza kutokana na kifo au ulemavu wa kudumu, pamoja na kuwasaidia kupanga na kutimiza malengo yao ya kifedha.

“Ni muhimu watumishi kupata uelewa kuhusu Bima ya Maisha ili waweze kufanya maamuzi sahihi katika kupanga maisha yao ya sasa na ya baadaye, pamoja na kulinda familia na wategemezi wao,” amesema Bi. Lwangili.

Katika hatua nyingine, Bi. Lwangili amewapongeza na kuwatakia watumishi wa Ofisi hiyo waliozaliwa mwezi Septemba baraka, afya njema, furaha na mafanikio zaidi, huku akiwashukuru kwa kujituma na kujitoa katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Amesema watumishi hao ni watu wa thamani katika Utumishi wa Umma, akiwaombea kuendelea kupata upendo na baraka za Mungu, kukua na kuwa baraka kwa familia zao, jamii na Utumishi wa Umma kwa ujumla.

Kwa upande wake Afisa Bima Mkuu kutoka Shirika la Bima ya Taifa Dodoma, Bi. Aurelia Joseph, amesema Bima ya Maisha ni mkataba kati ya mteja na kampuni ya bima, ambapo mteja hulipa ada ya bima kwa awamu au mkupuo na kupata stahiki endapo tukio lililowekewa bima litatokea, au kupata mafao yanayohusiana na akiba kulingana na aina na masharti ya bima.

Vilevile, Afisa Mauzo kutoka Shirika la Bima ya Taifa, Dar es Salaam, Bw. Omary Mchimbi, ameeleza aina mbalimbali za Bima ya Maisha zinazotolewa na Shirika hilo, ikiwemo Bima ya Beamlife, Bima ya Elimu, Bima ya Maisha, Bima ya Malengo na Bima ya Matumaini, ambazo hutoa fursa za kuweka akiba, kulinda wategemezi na kutimiza malengo mbalimbali ya kifedha, kwa mujibu wa masharti ya kila mkataba.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili, akizungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo (hawapo pichani) wakati alipokuwa akihitimisha mafunzo kuhusu Bima ya Maisha yaliyotolewa na wawezeshaji kutoka Shirika la Bima ya Taifa (NIC) Septemba 28, 2026 jijini Dodoma



Baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi. Prisca Lwangili (hayupo pichani) wakati akihitimisha mafunzo kuhusu Bima ya Maisha yaliyotolewa na wawezeshaji kutoka Shirika la Bima ya Taifa (NIC) tarehe 28 Septemba, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma

Viongozi na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya uelewa kutoka kwa wawezeshaji wa Shirika la Bima ya Taifa (NIC) (hawapo pichani) wakati walipokuwa wakitoa maelezo kuhusu Bima ya Maisha tarehe 28 Septemba, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma

Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakiimba wimbo wa pongezi kwa watumishi wenzao waliozaliwa mwezi Septemba, katika kumbukizi ya siku zao za kuzaliwa, mara baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bi. Prisca Lwangili kuhitimisha mafunzo kuhusu Bima ya Maisha yaliyotolewa na wawezeshaji kutoka Shirika la Bima ya Taifa (NIC) Jijini Dodoma.

Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi. Prisca Lwangili (hayupo pichani) wakati akihitimisha mafunzo kuhusu Bima ya Maisha yaliyotolewa na wawezeshaji kutoka Shirika la Bima ya Taifa (NIC) tarehe 28 Septemba, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma

Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi. Prisca Lwangili (hayupo pichani) wakati akihitimisha mafunzo kuhusu Bima ya Maisha yaliyotolewa na wawezeshaji kutoka Shirika la Bima ya Taifa (NIC) tarehe 28 Septemba, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (wa tatu kutoka kushoto) akifuatilia mada ya mafunzo kuhusu Bima ya Maisha iliyotolewa na Maafisa kutoka Shirika la Bima ya Taifa (NIC) leo Septemba 28, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma.

Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi. Prisca Lwangili (hayupo pichani) wakati akihitimisha mafunzo kuhusu Bima ya Maisha yaliyotolewa na wawezeshaji kutoka Shirika la Bima ya Taifa (NIC) tarehe 28 Septemba, 2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma


Afisa Bima Mkuu kutoka Shirika la Bima ya Taifa (NIC), Bi. Aurelia Joseph, akitoa neno la utangulizi na kueleza dhana ya Bima ya Maisha kwa Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo, Mtumba Jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mussa Magufuli akifafanua jambo kwa Watumishi wa Ofisi hiyo mara baada ya  wawezeshaji kutoka Shirika la Bima ya Taifa (NIC) kutoa mafunzo kuhusu Bima ya Maisha katika eneo maalumu la Ofisi hiyo septemba 28, 2026 jijini Dodoma

Afisa Mauzo kutoka Shirika la Bima ya Taifa (NIC) Bw. Omary Mchimbi, akielezea aina mbalimbali za Bima ya Maisha zinazotolewa na Shirika hilo kwa Viongozi na Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa Mafunzo ya uelewa kuhusu Bima ya Maisha yaliyotolewa Septemba 28, 2026 katika Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma





No comments:

Post a Comment