Friday, August 14, 2026

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAIPONGEZA TASAF KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO, YASISITIZA KUENDELEZA UWAZI NA UWAJIBIKAJI KATIKA KUFIKIA WALENGWA WALIOKUSUDIWA ILI KUTIMIZA MALENGO YA PSSN III

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 14 Agosti, 2026 

Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepokea taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III) na kutoa maelekezo ya kuendeleza misingi ya utekelezaji wenye ufanisi, uwazi na uwajibikaji katika kufikia walengwa waliokusudiwa na kutimiza malengo ya PSSN III.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amezungumza hayo leo tarehe 14 Agosti, 2026 Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akiongoza kikao cha Kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kilicholenga kupokea taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III).

Vilevile, Mhe. Dkt. Ndumbaro ameipongeza TASAF kwa utekelezaji mzuri wa Miradi ya Maendeleo ikiwemo ujenzi kwenye sekta ya elimu na afya.

“Kwa niaba ya Kamati yangu nitoe pongezi nyingi kwa ofisi hii, kwa hakika mnafanya kazi nzuri katika mpango wa kunusuru kaya maskini, lakini pia mnatekeleza vizuri Miradi ya Maendeleo ikiwemo ujenzi  kwenye sekta ya elimu na afya, mnamwakilisha vizuri Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa miradi hii’’ Amesema Mhe. Dkt. Ndumbaro

Awali akiwasilisha kwa Kamati hiyo taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III), Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray amesema, PSSN III iliidhinishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Dunia tarehe 10 Aprili 2026, na kwa sasa ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha maandalizi kabla ya kuanza utekelezaji.

Naibu Waziri Qwaray amesema kuwa, katika maandalizi ya utekelezaji wa PSSN III, hatua muhimu zimekamilika ikiwemo kukamilisha usanifu wa Mpango, kuandaa nyaraka mbalimbali za utekelezaji, miongozo ya kiutendaji na kuimarisha mifumo ya TEHAMA inayosimamia shughuli za Mpango.

Aidha ameongeza kuwa, mchakato wa utambuzi wa Mamlaka za Maeneo ya Utekelezaji yatakayoshiriki kwenye utekelezaji wa Mpango unaendelea na unaojumuisha timu ya wataalamu kutoka TASAF, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS), pamoja na wataalamu wa mazingira ambapo uchambuzi na uchakataji huo utazingatia viwango vya umaskini katika ngazi ya Halmashauri pamoja na viashiria vya athari za kimazingira, ikiwemo uwezekano wa maeneo kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi na majanga mbalimbali.

Vilevile, Mhe. Qwaray amesema kupitia mpango huo unatarajiwa kuongeza uwezo wa kaya maskini na zilizo katika mazingira hatarishi kukabiliana na changamoto za kiuchumi, kijamii na kimazingira, kuongeza ujuzi na taaluma kwa vijana kutoka kaya maskini na zinazoishi katika mazingira hatarishi zitakazoweza kujiajiri na kuajiriwa, kuwa na masijala ya kitaifa (kanzi data) yenye taarifa muhimu ya kaya maskini na zilizopo katika mazingira hatarishi pamoja na urasimishwaji wa TASAF kama taasisi ya umma ya kutekeleza na kusimamia utoaji wa huduma za msaada ya kijamii itakayohakikisha uendelevu, ufanisi na uratibu wa utoaji wa huduma hizo nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Bw. Shedrack Mziray ameishukuru Kamati hiyo kwa maoni na ushauri mbalimbali ambao wameutoa na kuahidi kufanyia kazi ili kuimarisha na kuboresha utendaji kazi wa Taasisi hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Kamati yake kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kilicholenga kupokea taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III).


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (aliyesimama kulia) akiwasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III). Wengine ni Viongozi na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akifurahia jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na ofisi hiyo kilicholenga kuwasilisha taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III).


Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Bw. Shedrack Mziray akisikiliza maoni kutoka kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao cha Kamati hiyo Bungeni jijini Dodoma na Watendaji hao kilicholenga kuwasilisha taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III).


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Nyamizi Mhoja akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Kamati hiyo na ofisi hiyo kilicholenga kuwasilisha taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III).

Viongozi na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma kilicholenga kuwasilisha taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III).


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Sikudhani Chikambo akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Kamati hiyo na ofisi hiyo kilicholenga kuwasilisha taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III).


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akifafanua hoja Bungeni jijini Dodoma wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na ofisi hiyo kilicholenga kuwasilisha taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III).


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (kushoto) wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na ofisi hiyo kilicholenga kuwasilisha taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III).

Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (aliyesimama) akifafanua hoja iliyowasilishwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao cha Kamati hiyo na ofisi hiyo kilicholenga kuwasilisha taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III).


Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Bw. Shedrack Mziray (kulia) akiandika maoni yaliyokuwa yakiwasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kilicholenga kuwasilisha taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III). Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, SACP. Ibrahim Mahumi. 


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (aliyesimama mbele) akiwasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III). Wengine ni Viongozi na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora.


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Saashisha Mafuwe akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Kamati hiyo na ofisi hiyo kilicholenga kuwasilisha taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III).


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Yohana Msita akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Kamati hiyo na ofisi hiyo kilicholenga kuwasilisha taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III).

Sehemu ya Wakurugenzi na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia jambo wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza kwenye kikao Bungeni jijini Dodoma mara baada ya Watendaji wa ofisi hiyo kuwasilisha taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III).

Sehemu ya Wakurugenzi Wasaidizi na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia jambo wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza kwenye kikao Bungeni jijini Dodoma mara baada ya Watendaji wa ofisi hiyo kuwasilisha taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III).






No comments:

Post a Comment