Monday, August 10, 2026

NAIBU KATIBU MKUU LWANGILI ASISITIZA UJUZI NA HAIBA YA UONGOZI KATIKA URITHISHANAJI MADARAKA KWA WATUMISHI WA UMMA

Na Antonia Mbwambo - Dodoma

Tarehe 10 Agosti, 2026

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kujenga ujuzi wa kitaalamu na haiba ya uongozi katika kuwaandaa warithi wa madaraka ili kuhakikisha kunakuwa na mwendelezo wa utendaji na utoaji wa huduma bora katika Taasisi za umma.

Bi. Lwangili ameyasema hayo leo, Agosti 10, 2026, wakati akihitimsha mafunzo ya uelewa kuhusu Urithishanaji Madaraka yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Mtumba Jijini Dodoma.

Amesema maandalizi ya urithishanaji madaraka yanapaswa kuanza mapema kwa kuwajengea uwezo unaohitajika katika nafasi za uongozi wanazotarajiwa kuzishika.

Aidha, Bi. Lwangili ameongeza kuwa ujuzi wa kitaalamu (Technical Skills) humwezesha Mtumishi kuwa na maarifa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, huku haiba ya uongozi ikimsaidia kuwasiliana vizuri, kujiamini, kushirikiana na wengine, kuwa mwadilifu, kufanya maamuzi na kuwajibika.

“Kuwa na ujuzi wa kitaalamu pekee hakutoshi. Mtumishi anayejengwa kuwa Kiongozi wa baadaye anapaswa pia kuwa na haiba inayomjengea uwezo wa kuwasiliana vizuri, kujiamini, kushirikiana na wengine, kuwa mwadilifu, kufanya maamuzi na kubeba majukumu kwa uwajibikaji,” amesema Bi. Lwangili.

Pia Bi. Lwangili amesisitiza kuwa, Urithishanaji Madaraka si kumwandaa mtu kuchukua nafasi ya Kiongozi aliyepo pekee, bali ni kuimarisha Taasisi kwa kuwa na Watumishi wenye uwezo wa kuendeleza majukumu na huduma za umma.

Kwa upande wake, Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Bertha Bomani, ameeleza kuwa Urithishanaji Madaraka ni mchakato wa kuwaandaa mapema Watumishi wenye uwezo na sifa stahiki kwa ajili ya majukumu ya uongozi.

Bi. Bomani amebainisha mikakati ya Urithishanaji Madaraka katika Utumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu ya uelewa na kujenga uwezo kwa Viongozi na Watumishi kuhusu manufaa ya kuandaa na kutekeleza Mpango wa Urithishanaji Madaraka, pamoja na kuwakumbusha Waajiri kutenga fedha katika bajeti za Taasisi zao kwa ajili ya uandaaji na utekelezaji wa mpango huo.

 

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili akizungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo (hawapo pichani) wakati Naibu Katibu Mkuu huyo akihitimisha Mada ya mafunzo kuhusu Urithishanaji wa Madaraka leo tarehe 10 Agosti, 2026 Mtumba Jijini Dodoma.


Baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya Uelewa kuhusu Urithishanaji Madaraka yaliyofanyika tarehe 10 Agosti,2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo iliyopo Mtumba Jijini Dodoma

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (aliyesimama mbele) akizungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo wakati Naibu Katibu Mkuu huyo akihitimisha Mada ya mafunzo kuhusu Urithishanaji wa Madaraka leo tarehe 10 Agosti, 2026 Mtumba Jijini Dodoma

Baadhi ya Watumishi kutoka Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya Uelewa kuhusu Urithishanaji Madaraka yaliyofanyika tarehe 10 Agosti,2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo iliyopo Mtumba Jijini Dodoma

Baadhi ya Watumishi kutoka Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya Uelewa kuhusu Urithishanaji Madaraka yaliyofanyika tarehe 10 Agosti,2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo iliyopo Mtumba Jijini Dodoma

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (wa pili kutoka kulia) akifuatilia mafunzo ya uelewa ambayo hutolewa kila jumatatu ya wiki katika eneo maalumu la Ofisi hiyo Mtumba Jijini Dodoma leo tarehe 10, Agosti, 2026. Wengine ni Wakurugenzi na Wakurugenzi wasaidizi wa Idara na Vitengo vya Ofisi hiyo.

Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Leila Mavika akitoa ufafanuzi kuhusu Urithishanaji Madaraka mara baada ya muwezeshaji ambaye pia ni Mchumi Mkuu wa Ofisi hiyo, Bi. Bertha Bomani, kutoa maelezo kuhusu mada hiyo leo tarehe 10 Agosti, 2026 Jijini Dodoma

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (wa kwanza kutoka kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini Bw. Priscus Kiwango (wa pili kutoka kushoto) wakati wa mafunzo ya uelewa kwa Watumishi wa Ofisi hiyo yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi hiyo iliyopo Mtumba Jijini Dodoma


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (wa kwanza kutoka kulia) akifuatilia mafunzo kuhusu Urithishanaji Madaraka kutoka kwa Mchumi Mkuu Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Bi. Bertha Bomani leo tarehe 10 Agosti, 2026 Mtumba jijini Dodoma. Kulia kwake ni Wakurugenzi na Wakurugenzi wasaidizi wa Vitengo vya Ofisi hiyo.

Baadhi ya Wakurugenzi wasaidizi na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya Uelewa kuhusu Urithishanaji Madaraka yaliyofanyika tarehe 10 Agosti,2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo iliyopo Mtumba Jijini Dodoma


Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Bertha Bomani, akielezea dhana ya Urithishanaji Madaraka kwa Watumishi wa Ofisi hiyo wakati wa Mafunzo ambayo hufanyika kila jumatatu ya wiki kwa lengo la kuwajengea Watumishi hao uwezo wa kiutendaji Mtumba Jijini Dodoma

Baadhi ya Viongozi na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya Uelewa kuhusu Urithishanaji Madaraka yaliyofanyika tarehe 10 Agosti,2026 katika eneo maalumu la Ofisi hiyo iliyopo Mtumba Jijini Dodoma


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili (wa kwanza kutoka kushoto) akisalimiana na baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi hiyo, mara baada ya Naibu Katibu Mkuu huyo kuhitimisha mafunzo ya uelewa kuhusu Urithishanaji Madaraka yaliyofanyika Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment