Wednesday, August 12, 2026

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAPOKEA TAARIFA YA UTENDAJI WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA, YASISITIZA UTOAJI WA ELIMU KUHUSU RUFAA NA MALALAMIKO KWA WATUMISHI WA UMMA

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 12 Agosti, 2026


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepokea taarifa ya utendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma na kusisitiza kutolewa kwa elimu zaidi kwa Watumishi wa Umma ili waweze kuwasilisha rufaa na malalamiko kwa wakati na mahali husika kwa lengo la kutimiza haki na wajibu katika utendajikazi.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro alipokuwa akiongoza kikao cha Kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Tume ya Utumishi wa Umma kilicholenga kupokea taarifa ya Utendaji wa Tume hiyo katika kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira.

“Elimu inahitajika zaidi kwa Watumishi wa Umma kwenye maeneo yao ya kazi ili kuongeza uelewa wa namna ya kushughulikia rufaa na malalamiko hayo ikiwa ni pamoja na kupata utatuzi wa migogoro katika Utumishi wa Umma,’’ Amesisitiza Mhe. Dkt. Ndumbaro

Katika hatua nyingine, Mhe. Dkt. Ndumbaro amempongeza na kumshukuru Waziri Kikwete kwa taarifa nzuri aliyoiwasilisha kwa Kamati hiyo iliyoelezea kwa kina taarifa ya utendaji ya Tume ya Utumishi wa Umma katika kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira ambayo itaongeza chachu ya utendaji kazi kwa Watumishi wa Umma.

Mhe. Dkt. Ndumbaro ameiahidi Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kuwa itashirikiana nayo katika usimamizi wa masuala mbalimbali ili kuleta matokeo chanya kwa ustawi wa Taifa.

Awali akiwasilisha kwa Kamati hiyo taarifa ya utendaji ya Tume ya Utumishi wa Umma katika kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema, Tume ya Utumishi wa Umma ni Mamlaka ya Rufaa kwa Watumishi wa Umma katika taasisi 554 waliopo kwenye makundi mbalimbali ya Watumishi wa Umma, Serikali Kuu, Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Watumishi waliopo katika Taasisi za Umma.

Vilevile, Mhe. Kikwete amesema Tume hiyo ina jukumu la kupokea malalamiko na rufaa kutoka kwa Watumishi wa Umma ambao hawakuridhika na uamuzi wa mamlaka zao za ajira, mamlaka za nidhamu na waajiri baada ya uamuzi walioufanya na mamlaka hizo hivyo, elimu itakayotolewa kwa Watumishi wa Umma itasaidia kwa kiasi kikubwa kupata haki na wajibu kwa kila mmoja.

Aidha, Mhe. Kikwete ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kwa kuwa na majadiliano mazuri na ofisi anayoiongoza ambayo wanaamini yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza ufanisi na utendaji wa majukumu yao.

“Mhe. Mwenyekiti, nitoe shukrani za dhati kwa niaba ya ofisi ninayoiongoza mara zote tumepokea maoni, ushauri na michango mbalimbali kutoka katika Kamati yako inayolenga kuboresha Utumishi wa Umma nchini kwa lengo la kutimiza azma ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na Utumishi wa Umma uliotukuka.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amesema Kamati hiyo imekuwa msaada mkubwa wa kuiongoza Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kwa kuwapatia maarifa mengi kutoka kwa Wajumbe wote wa Kamati hiyo yenye kuleta tija katika kuwahudumia wadau mbalimbali na kuboresha utendajikazi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (aliyesimama) akizungumza wakati wa kikao cha Kamati yake kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Taasisi ya Tume ya Utumishi wa Umma baada ya Tume hiyo kuwasilisha taarifa kuhusu kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira.




Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza wakati wa kikao cha Kamati yake kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Taasisi ya Tume ya Utumishi wa Umma baada Tume hiyo kuwasilisha taarifa kuhusu kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwasilisha kwa Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria taarifa ya kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira wakati wa kikao kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma. Wengine ni Viongozi na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwasilisha kwa Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria taarifa ya kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira wakati wa kikao kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma. Wengine ni Viongozi na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI


Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia jambo wakati wa kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI kilicholenga kutoa taarifa ya kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akiwa katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI kilicholenga kutoa taarifa ya kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa ofisi yake Mhe. Regina Qwaray.


Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa kwenye kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI kilicholenga kutoa taarifa ya kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira.


Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia jambo wakati wa kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI kilicholenga kutoa taarifa ya kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira.


Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa kikao cha Kamati hiyo Bungeni jijini Dodoma na Watendaji hao kilicholenga kutoa taarifa ya kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akifafanua hoja Bungeni jijini Dodoma wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilicholenga kuwasilisha taarifa ya kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira.


Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nolasco Kipanda (aliyesimama) akisikiliza maoni kutoka kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao cha Kamati hiyo Bungeni jijini Dodoma na Watendaji hao kilicholenga kutoa taarifa ya kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira.

Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (aliyesimama) akifafanua hoja iliyowasilishwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kilicholenga kuwasilisha taarifa ya kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili akishukuru baada ya kupokea pongezi kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ya kuteuliwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo. Pongezi hizo zimetolewa baada ya kikao cha Kamati hiyo na Watendaji wa ofisi hiyo kilicholenga kutoa taarifa ya kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira.


Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia jambo wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha Kamati hiyo Bungeni jijini Dodoma na Watendaji hao kilicholenga kutoa taarifa ya kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira.


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Edwin Swalle (wa kwanza kulia) akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa kikao kilicholenga kuwasilisha taarifa ya kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma.


Watendaji na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia jambo wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha Kamati hiyo Bungeni jijini Dodoma kilicholenga kutoa taarifa ya kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira.


Watendaji na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia jambo wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha Kamati hiyo Bungeni jijini Dodoma kilicholenga kutoa taarifa ya kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira.



 

No comments:

Post a Comment