Friday, March 1, 2019

DKT. MWANJELWA AMTAKA MKURUGENZI MTENDAJI MAFIA KUPUNGUZA SAFARI ILI AKAE OFISINI KUFANYA KAZI



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia (hawapo pichani), wakati wa kikao kazi na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji. 

Baadhi ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao kazi chenye  lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao. 

Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Mhe. Shaibu Nnunduma  akimkaribisha wilayani Mafia, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika wilaya hiyo. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Bw. Erick C. Mapunda akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya halmashauri yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kabla ya kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa halmashauri hiyo chenye lengo la  kuhimiza uwajibikaji. 

Mbunge wa Jimbo la Mafia, Mhe. Mbaraka Dau akiwasilisha changamoto zinazowakabili watumishi wa umma katika jimbo lake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kabla  ya kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia chenye lengo la  kuhimiza uwajibikaji. 

No comments:

Post a Comment