Wednesday, March 27, 2019

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AIPONGEZA OFISI YA RAIS - UTUMISHI KWA KUKAMILISHA UJENZI WA OFISI YAKE KWA WAKATI KWENYE MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akizungumza  na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kwenye mji wa serikali, mara baada ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akifurahia jambo mara baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kwenye mji wa serikali, mara baada ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akiwa ndani ya ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) iliyopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitoa neno la shukrani kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb), mara baada ya Mhe. Majaliwa kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) na ujumbe wake wakiwasili katika jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Muonekano wa jengo jipya  la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael wakifurahia jambo na viongozi wengine mara baada ya kukamilika kwa ziara ya Mhe. Kassim M. Majaliwa ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment