Wednesday, June 22, 2016

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2016, MKOANI MANYARA

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bw. Eliakim Maswi akizungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Manyara katika kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Dkt. Joel Bendera akizungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Manyara katika kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa Watumishi wa Umma wa mkoa wa Manyara kuhusu hoja mbalimbali alizozipokea wakati wa kikao kazi cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mkoani Manyara.

Afisa Muuguzi Msaidizi, Mkoa wa Manyara,Bi. Josephine Mosha akiwasilisha maoni kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki wakati wa kikao kazi cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mkoani Manyara.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb), akikabidhiwa ripoti kuhusu kero na maoni kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Mkoa (CWT)-Manyara Bw. Qambos Michael Sulle ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
 

No comments:

Post a Comment