Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 inatoa huduma za kiutumishi katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni, 2025.
Hivyo,
Watumishi wa Umma na Wananchi wote wanakaribishwa kutembelea banda la ofisi
hiyo ili kupata huduma mbalimbali za kiutumishi.
Baadhi
ya huduma hizo ni Mifumo ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini,
e-Watumishi (HCMIS), e-Msawazo (HR-Assessment), e-Uhamisho (Watumishi Portal),
e- Mikopo, e-Utendaji, e-Likizo na
e-Mrejesho.
Kadhalika, ofisi kwa kushirikiana na viongozi
wengine watashughulikia masuala ya PEPMIS.
Aidha, katika banda hilo zitatolewa huduma nyingine mathalani huduma za kisheria
katika Utumishi wa Umma.
No comments:
Post a Comment